ULEGA ATOA MWEZI MMOJA KWA TARURA KUHAKIKISHA UJENZIWABARABARA UMEKALIKA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 2, 2021

ULEGA ATOA MWEZI MMOJA KWA TARURA KUHAKIKISHA UJENZIWABARABARA UMEKALIKA

 
Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambae ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mkuraga mkoa wa Pwani  tarehe 1 Februari 2021. wakati wa ziara ya kukangua miradi mbalimbali ujenzi wa barabara na ujezi wa daraja la Kifaurongo lilitopo kata ya Tambani ambapo ametoa mwezi mmoja kwa tarura kuhakikisha ujenzi wabarabara ya Vikindu Sangatini umekalika.(Picha na Emmanuel Massaka wa MIchuzi Tv)
 
Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambae ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega (kulia) akizungumza na wananchi wa kata ya Tambani ambapo amewaomba wananchi kulinda vifaa vyote vinavyotumika kujengea daraja la Kifaurongo. jana tarehe 1 Februari.
 
Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambae ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega (kulia) akiwa na viongozi wa mbalimbali wa wilaya hiyo wakikaguwa ujezi wa daraja Kifaurongo lilipo kata ya Tambani.
 
 
Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambae ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega (kushoto akimsikiliza mwananchi  wati wa ziara ya kukaguwa ujezi wa barabara ya Vianzi Sangatini kata ya Vikindu.
Kazi ikiendelea Ujezi wa daraja la Kifaurongo kata ya Tambani
 
 
Kazi ikiendelea ya ujezi wa barabara ya Vianzi Sangatini kata ya Vikindu
 


 

*********************************

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye ni Naibu Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na michezo ,Abdalah Ulega ametoa mwezi mmoja kwa tarura wilaya ya mkuranga kuahakikisha barabara ya vikindu sangatini ambayo inajengwa iwe imekamilika.

 

Ulega ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa Barbara hiyo katika kata ya vikindu wilayani mkuranga mkoani pwani na kuwasisitiza wakandarasi kutumia pesa za mradi vizuri katika malengo yaliyo kusudiwa.

 

Amesema kuanzia kesho mkandarasi hakikishe ananza kuchimba mitaro sambamba nakuweka mawe pembezoni mwakuta za barabara ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea  mvua za masika zitakapoanza.

 

"Hapa mvua zikianza kunyesha kabla mitaro haijachimbwa hii barabara itakatika na nyumba zilizopembezoni zitaanguka, kwahiyo tarura shughulikieni ili suala haraka sambamba nakuweka barabara za mchepuko kwa ajili ya kupunguza msongamano wamagari." Amesema ulega

 

Aidha ulega ameongeza kuwa mkandarasi aliyekuwepo saiti alipewa miezi nane kazi iweimekamilika,lakini mpaka sasa ni miezi saba hakuna kilichofanyika hivyo ametaka kazi hiyo ikamilike ndani ya mwezi mmoja uliobaki.

 

Kwa upande wake Mhandis Bernard Mwita akizungumza kwa niaba ya meneja wa tarura mhandis Godfrey Mlowe amesema mkandarasi waliempa kazi ndiye aliyewakwamisha ila watahakikisha kazi hiyo inakamilika kwa wakati.

 

Kwa upande wake diwani wa kata ya vikindu Mohammed Maundu amemshukuru mbunge wa jimbo hilo kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kutatua changamoto za wananchi.

 

Katika hatua nyingine ulega ametembelea ujenzi wa daraja la kifaurongo lilopo tambani mkuranga mkoani pwani na kumtaka meneja wa tarura kuhakikisha karavati linalojengwa linakamilika kabla ya mvua za masika kuanza ili kuondoa kero kwa wananchi.

 

Akizungumza mbele ya wananchi wakati wa ziara yake katika kata ya tambani ulega amemsisitiza meneja watarura kuhakikisha kunajengwa karavati kubwa  litakalo weza kuhimili maji yanayopita kwa kasi.

 

Ujenzi wa daraja la kifaurongo ambalo linaunganisha mkoa wa Dar es salaam

Kwa wilaya ya temeke kupitia mbande, na mkoa wa pwani kwa wilaya ya mkuranga kupitia kata ya tambani,litawasaidia sana wananchi kwani kipindi cha mvua eneo hilo halipitiki hali inayopelekea wananchi kuvuka na madumu kitendo kinacho hatarisha maisha yao.

 

Hata  hivyo serikali ya awamu ya tano ya Daktari John Pombe Magufuli kupitia mbunge wa jimbo la mkuranga ilijenga daraja la kifaurongo lililogharimu kiasi cha mil 200 lakini kwa bahati mbaya liharibiwa na  mvua zilizopita, na imetoa  mil 200 zingine kwa ajili ya ukarabati wa daraja hilo ili kufanya kero hiyo kuwa historia kwa wananchi wa kata ya tambani

 

Awali ulega alishiriki uchimbaji msingi wa ujenzi wa madarasa matatu kwa shule ya msingi shikizi ya mpera iliyopo kata ya vikindu wilayani mkuranga mkoani pwani, ambapo amekabidhi mabati 100 na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kumalisha ujenzi huo.

 

Akikabidhi mabati hayo Abdalah Hamisi ulega ambaye pia ni naibu waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo amesema ujenzi wa shule hiyo ni muhimu kwasababu itapungunza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi katika shule ya msingi kisemvule.

Naye diwani wa kata ya vikindu Mohammed Maundu amesema shule hiyo shikizi ikikamilika itachukua watoto wa darasa la kwanza hadi la tatu kwa sasa ili kuwapunguzia changamoto vivuko na umbali.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad