BILIONI 2 ZAKUSANYWA WILAYANI KALIUA KATIKA MIEZI SITA YA MWAKA WA FEDHA UNAOENDELEA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 2, 2021

BILIONI 2 ZAKUSANYWA WILAYANI KALIUA KATIKA MIEZI SITA YA MWAKA WA FEDHA UNAOENDELEA

                                                                           

Mwenyekiti wa Halamashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua  Japhael Lufungija akitoa taarifa jana ya utekelezaji kwa kipindi miezi sita iliyopita .
Mwenyekiti wa Halamashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua  Japhael Lufungija akitoa taarifa jana ya utekelezaji kwa kipindi miezi sita iliyopita .
Mwenyekiti wa Halamashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua  Japhael Lufungija akitoa taarifa jana ya utekelezaji kwa kipindi miezi sita iliyopita .

Baadhi ya Majumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwa katika kikao cha kupitia hoja na taarifa za utekelezaji wa Kamati mbalimbali jana.

 

Baadhi ya Majumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwa katika kikao cha kupitia hoja na taarifa za utekelezaji wa Kamati mbalimbali jana.*************************

NA TIGANYA VINCENT

RS TABORA 

2 FEBRUARI 2021

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 2  kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha unaoendelea.

Kiasi hicho cha fedha ni sawa na asilimia 67.1 ya makisio ya shilingi bilioni 3 ya ambayo Halmashauri hiyo imepanga kukusanya ndani ya mwaka huu wa fedha.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Japhael Lufungija wakati akitoa taarifa za utekelezaji wa shughuli kwa kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Aliwataka Watendaji  kuhakikisha wanaongeza kasi ,uadilifu katika ukusanyaji wa mapato ili hatimaye waweze kuvuka asilimia 100 ya lengo na kupata fedha nyingi zitakazosaidia kuboresha upelekaji wa huduma mbalimbali kama vile elimu na afya kwa wananchi.

Lufungija alisema katika kipindi hicho, Halmashauri hiyo imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 290 kwa vikundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani. 

Alisema kati ya fedha shilingi milioni 156 zimetolewa kwa vikundi 17 vya vijana  na shilingi 119 zimetolewa kwa vikundi 23 vya wanawake  na shilingi milioni 15 zimetolewa kwa vikundi vitano vya watu wenye ulemavu. 

Lufungija alivitaka vikundi vilivyokopeshwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na kwa kufauta utaratibu ili vikundi vingi viweze kunufaika na fedha hizo.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika kipindi hicho Halmashauri hiyo imeendelea na ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya shule za Msingi na sekondari ambavyo vimegharimu shilingi milioni 147.

Aliongeza kuwa pia wameweza kugawa bati 1,692 kati ya 4,308 katika Kata ambazo zilikuwa zimekamilisha Maboma ya Shule na kukamilisha ununuzi wa mbao na vifaa vinavyohusiana na upauaji ikiwemo malipo ya fundi.

Lufungija alisema hivi sasa wanaendelea na ugawaji bati kwa miradi inayokidhi vigezo kwa lengo la kushirikiana na wananchi kupunguza uhaba wa miundombinu shuleni.

Alisema sanjari na ugawaji bati pia wameweza kutoa mifuko ya saruji 1,410 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyuma 10 katika maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad