Kaimu
mkurungenzi mkuu Wa Tume ya Atomiki Tanzania,Dk Justine Ngaile( watatu
kulia waliokaa kwenye viti) akiwa na maofisa 40 wanaofanya mafunzo ya
kitaifa ya ukaguzi wa mizigo kwa kutumia mionziWashiriki wa mafunzo ya kitaifa ya ukaguzi wa mizigo kwa kutumia mionzi.

Washiriki wa mafunzo ya kitaifa ya ukaguzi wa mizigo kwa kutumia mionzi
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) Dk.Justine
Ngaile(aliyesimama) akifungua mafunzo ya kitaifa ya wiki moja kwa
wafanyakazi wanaotumia mionzi kukagua mizigo katika maeneo mbali mbali
nchini,ambapo mafunzo hayo yanafanyika makao makuu ya Tume jijini
Arusha.
TUME
ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) inaendesha mafunzo ya kitaifa kwa
wafanyakazi wanaofanya kazi ya kukagua mizigo na bidhaa mbali mbali za
wageni wa ndani na nje katika kuzingatia usalama wa mionzi kwenye
maeneo yao ya kazi ili kujilinda na kuwalinda Watanzania dhidi ya
madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.
Mafunzo
haya ya siku tano yameanza leo jumatatu tarehe 01 Februari 2021, Makao
Makuu ya TAEC, Jijini Arusha, ambapo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Dkt Justine Ngaile alifungua mafunzo
hayo rasmi na kuwataka washiriki wote kuchukua hatua zote stahiki za
kiusalama wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ili kuboresha usalama.
Jumla
ya maofisa 40 kutoka katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu kama
barabara na mamlaka mbalimbali kama vile viwanja vya ndege, hotelini,
viwandani na bandarini wanashiriki mafunzo haya ya matumizi salama ya
teknolojia ya mionzi kwenye ukaguzi wa mizigo ili kujipatia ujuzi na
kuwa bora katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
“Naamini
kozi hii kama inavyojieleza itaweza kuwasaidia katika kujenga ujuzi na
ubora katika kuifanya kazi ya ukaguzi wa mionzi kwa usahihi na kuwakinga
watanzania dhidi ya mionzi ” Dkt. Ngaile amesema.
Dkt.
Ngaile amesema kuwa maofisa hao wana jukumu kubwa katika kuhakikisha
wanafanya kazi yao ya ukaguzi kwa kutumia mionzi kwa ueledi ili
kuhakikisha usalama kwani vifaa wanavyovitumia kama vile X-Ray ili
kugundua aina ya mizigo iliyobebwa ndani kwenye vifungashio ina mionzi
mikali, hivyo ni muhimu kuchukua taadhari za kiusalama ili kujilinda wao
wenyewe, mazingira, pamoja na wananchi dhidi ya athari zinazoweza
kusababishwa na mionzi.
Kwa
upande wake mratibu wa mafunzo hayo Bwana Atumaini Makoba amesema
mafunzo ya mwaka huu yamewalenga watendaji wengi zaidi ili kuongeza wigo
wa elimu na ushirikiano baina ya watumiaji wa vyanzo vya mionzi na
wadhibiti ili kuongeza usalama wa mionzi mahala pa kazi katika kulinda
wananchi na mazingira dhidi ya mionzi.
No comments:
Post a Comment