Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka Viongozi
ngazi Mitaa kuhakikisha wanashughulikia ipasavyo kero na changamoto
mbalimbali kwenye mitaa yao na kuhakikisha wanatoa taarifa mapema pale
wanapobaini Jambo lipo juu ya uwezo wao ili liwezekushughulikiwa na
ngazi za juu.
RC Kunenge amesema hayo wakati wa kikao chake na
Watendaji na Wenyeviti wa mitaa Jijini humo ambapo amesema ni Jambo la
fedhea kuona kiongozi wa ngazi ya juu anashughulikia kero ya mtaa wakati
wahusika wa ngazi ya mtaa wapo wanapeta.
Aidha RC Kunenge
amewaelekeza Watendaji wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia ipasavyo
ukusanyaji wa Mapato ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya Mapato,
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ambapo amesisitiza
ukusanyaji wa Mapato usiwe wa kero Wala wa kuua Biashara za watu.
Hata
hivyo RC Kunenge amewataka Viongozi wa Mitaa kusimamia ipasavyo suala
la usafi wa mazingira kwenye mitaa yao ili kuwakinga wananchi na
magonjwa ya Mlipuko.
Pamoja na hayo RC Kunenge amewasisitiza pia
Viongozi hao kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa watu
wanaohatarisha usalama ikiwemo kufichua nyumba zinazogeuzwa Madanguro,
wanaowahifadhi wahamiaji haramu, wanaowatumia walemavu kujinufaisha na
wauzaji wa dawa za kulevya.
Sanjari na hayo amezielekeza Taasisi
za umma zilizopo jiji humo kuhakikisha wanashirikiana na Watendaji wa
Mitaa kwakuwa hao ndio wapo karibu na wananchi na ndio wanaozijua zaidi
kero za mtaa yao.
Mkutano huo baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam na Viongozi mbalimbali wa Mitaa umedhaminiwa na Bank ya CRDB
chini ya Kauli mbiu isemayo "UWAJIBIKAJI WA PAMOJA NI CHACHU YA
MAENDELEO YA MKOA WETU".
No comments:
Post a Comment