Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi ameongoza wananchi mbalimbali
wanaoishi FCkatika Kata ya Lwanwima kupanda miti ya maparachichi katika
Shule ya Msingi Lwanwima ikiwa ni sehemu ya kampeni ya wilaya hiyo
kuzifanya shule zote za kijani.
Kulingana na maelezo ya Afisa
Misitu wa wilaya hiyo, Deogratius Julius, kampeni hiyo inalenga kupanda
miti katika shule za sekondari na msingi na hata katika maeneo ya
taasisi za umma.
Hadi sasa wameshapanda miti 41,996 katika kipindi hiki cha mvua.
Wadau
mbalimbali wa mazingira walishiriki zoezi hilo wakiwemo Aga Khan Healrh
Services kupitia mradi wake wa Impact kanda ya ziwa ambao walikabidhi
miche 280 ya maembe na maparachichi
Picha mbalimbali katika kampeni ya upandaji miti ya miparachichi katika wilaya ya Nyamagana.
No comments:
Post a Comment