MJI WA KIBAHA WAPITISHA BAJETI YA BILIONI 36.2 KWA MWAKA 2021/2022 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 5, 2021

MJI WA KIBAHA WAPITISHA BAJETI YA BILIONI 36.2 KWA MWAKA 2021/2022

 Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Kibaha Mji mkoani Pwani, limepitisha bajeti ya mapato ya matumizi kwa mwaka 2021-2022 kiasi cha sh. bilioni 36.220 katika vyanzo mbalimbali vya mapato .

Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Selina  Wilson alisema kiasi
hicho mapato ya ndani ni sh. bilioni 3.937 na ruzuku toka Serikalini
ni sh.bilioni 31.734.724 .

Kati ya bajeti hiyo iliyopitishwa pia sh.bilioni 22.237  ni mishahara
na bilioni 1.299.312 ni matumizi ya kawaida ambapo miradi ya maendeleo
itatumia sh.bilioni 8.198.390.263.

Akizungumza katika baraza hilo, diwani wa kata ya Kongowe Hashim
Shomari alisema wameanza ujenzi wa kituo cha afya eneo la Miembe Saba
shule  kwa nguvu za wananchi ili kuondoa kero ya kufuata huduma mbali
hospital ya Tumbi hospital ya wilaya ya Lulanzi au Mkoani ambako
wanafuata huduma hiyo sasa .

Shomari aliiomba ,halmashauri iangalie namna ya kuunga mkono juhudi
hizo baada ya wananchi kuonyesha nia.

Kwa upande wake diwani wa viti maalum Lydia Mgaya alitaka wadau
mbalimbali washirikishwe katika kuchangia sekta ya elimu ili kupunguza
changamoto zilizopo.

Diwani wa kata ya Pichandege Karim Mtambo alieleza itakuwa vyema
endapo kitaboreshwa stendi kuu ya mabasi kwa kuweka vivutio, taa za
kutosha na kuwaondoa wasioendeleza viwanja eneo linalozunguka stendi
hiyo .

Doris Michael ambaye ni diwani viti maalum aliomba, elimu itolewa
kuhusiana na mabadiliko ya utaratibu mpya wa mikopo kwa vifaa badala
ya fedha kwa baadhi ya miradi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad