Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni wa kulia
Katibu
tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni (kulia) akizungumza na
baaadhi ya viongozi wa Chama cha soka Wilaya ya Bagamoyo (BFA)
walioongozwa na Mwenyekiti wao Olnjilie Maliwa wa kushoto kwa ajili ya
kuweka mikakati ya kuisaidia timu ya Bagafriends ambao ndio mabingwa wa
ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Pwani.
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
KATIKA kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kukuza sekta
ya michezo husaan mchezo wa soka Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo
Kasilda Mgeni amewaomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kwa
wingi kwa ajili ya kuisaidia kwa hali na mali timu ya soka ya Baga
friends ambayo ndio mabingwa wa ligi ya soka daraja la tatu ngazi ya
Mkoa wa Pwani ili ifanye vizuri katika hatua ya ligi ya mabingwa wa
Mkoa ngazi ya Taifa.
Mgeni ametoa rai hiyo wakati alipotembelewa na baadhi ya viongozi wa
Chama cha soka Wilaya ya Bgamoyo (BFA) Ofisni kwake pamoja na kamati
ya utendaji ya timu hiyo ya Bgafriends kwa ajili ya kuweza kuweka
mikakati amabyo itawesa kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika
hatua nyimgine inayofuata ya ngazi ya Taifa.
“Lengo la kukutana na viongozi hawa wa mpira wa miguu ambao wamekuja
ofisini kwangu wakiongozwa na Mwenyekiti wa BFA tuweze kujadili na
kuweka misingi imara ambayo itawasaidia wachezaji wetu ambao
wamepigana kufa na kupona katika kipindi chote na kufanikiwa kuwa
mabingwa wa ligi daraja la tatu ngani ya Mkoa wa Pwani kwa hivyo
tunapaswa kuwapa sapoti ya ina yake.
Katibu Tawala huyo amabye pia ni Mwenyekiti wa wa baraza la michezo
Wilaya Bagamoyo alifafanua kuwa timu hiyo kwa sasa ipo katika
maandalizi ya kujianda ana ligi ya mabingwa ngazi ya Taifa hivyo
serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa michezo inabidi
tunaweka mipango madhubuti ya kuhakikisha kwamba tunaweza kufika mbali
zaidi na kupanda daraja la pili na hatimaye katika siku zijazo tuweze
kushiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara.
“Hii timu imeweza kuutwaa ubingwa wa ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa
wa Pwani kwa hivyo kwa sasa inawakilisha Mkoa wa Pwani kwa ujumala
japo inatokea Wilaya ya Bgamoja kitu kikubwa ninachowaomba wadau wote
kwa pamoja tuungane na kutoa michango yetu ya fedha ambazo zitaweza
kutumika katika mahitaji mbali mbali ya chakula kwa wachezaji pamoja
na mambo mengine ya msingi kama mipira na jezi hivyo ninawaomba sana
na nia yetu tushiriki ligi kuu ya Tanzania bara katika siku ya
baadae.”alifafanua mgeni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha soka Wilaya ya Bagamoyo (BFA)
Olnjilie Maliwa alisema kwamba lengo kubwa na kwenda kumtembelea
katibu Tawala wa Wilaya hiyo juu ya timu yao ya soka y baga friends
ambayo imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi daraja la tatu katika ngazi
ya Mkoa wa Pwani ili kuweza mikakati ambayo itasaidia kuweza kufika
mbali zaidi katika hatua nyingine.
“Mimi kama Katibu wa BFA tumeweza kuongozana na uongozi wa kamati ya
utendaji ya mabingwa wetu wa soka katika ligi daraja la tatu ambao ni
timu ya Baga friends tukae kwa pamoja ili tuombe kituo ambacho
kitatumika kwa ajili ya michuano ya Taifa na lengo letu ni
kuhakikishatimu hii inaweza kufanya vizuri na kufika hatua ya ligi
daraja la pili katika msimu unaokuja.”alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Katika hatua nyingine alimponeza kwa dhati Katibu Tawala wa
wilaya ya Bagmoyo kwa kuwa bega kwa bega katika kipindi chote cha
michuano iliyopita hadi wameweza kufanikiwa kuibuka na ubingwa katika
ligi hiyo daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Pwani na kuwaomba wadau
wengine wa soka katika maeneo mbali mbali kujitokeza kwa wingi ili
kuipa sapoti ya kutosha timu yao ambayo ndio pekee inawakilisha Mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment