WATEJA wa Benki ya NMB wametakiwa kuchangamkia fursa za NMB Mastabata Siyo Kikawaida inayoelekea ukingoni, ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi za wiki pamoja na zawadi kuu 'Grande Finale,' inayojumuisha utalii wa ndani na bidhaa mbalimbali.
NMB Mastabata Siyo Kikawaida ni kampeni inayolenga kuhamasisha matumizi na manunuzi kwa Kadi za NMB Mastercard, Mastercard QR na POS, ilianza Novemba 24, 2020, ikitoa zawadi za Sh. 100,000 kwa washindi 40 kila wiki na washindi 12 wa zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 2.4 kila mwezi.
Akizungumza wakati wa droo ya 8 ya wiki ya kampeni hiyo, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara ya Kadi NMB - Lupia Matta, aliwataka wateja kuendelea kufanya manunuzi kwa njia ya kadi, ili kushinda zawadi kuu ya utalii wa ndani ambayo pia inampa mshindi fursa ya kuchagua zawadi mbadala.
Lupia alibainisha kuwa, washindi wa 'Grande Finale' inayotoa zawadi ya ziara ya utalii wa ndani katika mbuga za Serengeti, Ngorongoro ama Vsiwa vya Zanzibar, watakuwa huru kuchagua zawadi mbadala zilizotengwa zikiwa na thamani ya Sh. Milioni 8 kwa kila mmoja.
"Ziara ya washindi wetu wa 'Grande Finale' na wenza wao au rafiki, itakuwa ya siku tatu iliyolipiwa gharama zote, lakini wanapewa uhuru wa kuchagua zawadi mbadala ambazo ni TV kubwa iliyolipiwa kingamuzi cha DSTV miezi mitatu, friji kubwa, 'laptop', 'microwave', 'water dispenser na simu ya Samsung," alisema.
Aidha, aliongeza
kuwa NMB Mastabata Siyo Kikawaida imefanikiwa kwa asilimia zaidi ya 100, kwani
imeongeza idadi kubwa la watumiaji wa kadi katika manunuzi ya bidhaa, huku
akiahidi kuwa Benki yake itaendelea kubunii bidhaa bora zaidi zitakazorahisisha
upatikanaji wa huduma kwa wateja.
Katika droo hiyo, iliyofanyika Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, ikisimamiwa na Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) - Pendo Albert, jumla ya washindi 40 wa droo ya wiki hii walipatikana, ambako kila mmoja alijishindia Sh. 100,000/-.
Katika droo saba
zilizotangulia (saba za wiki na mbili za mwezi), pesa taslimu na zawadi
mbalimbali zenye thamani ya Sh. Milioni 114.8 zimetolewa, ambazo ukijumlisha na
Sh. Mil. 4 walizojishindia washindi 40 wa droo ya nane, thamani kuu inakuwa Sh.
Mil. 118.8.
No comments:
Post a Comment