HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 2, 2021

DKT NGENYA AWATAKA WAJASIRIAMALI WACHANGAMKIE FURSA TBS

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Dkt Yusuph Ngenya akizungumza na waandishi wa habari Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 Mjasiriali wa viungo anayesafirisha bidhaa hizo nchi za Ulaya kutoka Zanzibar, Khamis Issa Mohamed akizungumza na waandishi wa habari Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. 

Mwenyekiti wa kamati ya viwango wa TBS wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Dkt Stephen Nyandoro akizungumza na wandishi wa habari mjini Moshi.

 Ofisa mkuu wa viwango kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Stella Apolot akizungumza na waandishi wa habari juu ya faida za semina hiyo ya wajasiriamali Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wajasiriamali wa bidhaa za mbalimbali za kahawa, chai na viungo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa na TBS, EAC na GAZ yanayoendelea Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 

********************

Na Mwandishi wetu, Moshi

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Dkt Yusuph Ngenya amewataka wajasiriamali wadogo wadogo nchini kuchangamkia fursa ya kupatiwa alama ya ubora bila malipo kwenye shirika hilo ili bidhaa zao zikubalike ndani na nje ya nchi.

Dkt Ngenya ameyasema hayo mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mafunzo ya siku tano ya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Amesema wanavyo viwango vingi vya bidhaa za wajasiriamali wagodo hivyo wanawasaidia kuwapatia alama za ubora bila malipo kutokana na serikali kutenga fedha za kugharamia hayo.

“Wajasiriamali wadogo wadogo msiogope kuja kwetu TBS tuna mfumo wa kuwasaidia na nimesema hili mara nyingi kuwa wachangamkie fursa hii,” amesema Dkt Ngenya.

Ofisa mkuu wa viwango kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki, Stella Apolot amesema kupitia mafunzo hayo yaliyoandaliwa kupitia EAC, GAZ na TBS wadau watatambua namna ya kufanya katika kuandaa bidhaa bora zaidi ya viwango.

 

Apolot amesema wadau hao wanapaswa kutambua kuwa utekelezaji wa viwango unapaswa kuwa rahisi kwa walaji na wasiwe watumiaji pekee.

 

Mwenyekiti wa kamati ya viwango wa TBS wa chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM, Dkt Stephen Nyandoro amesema anatarajia washiriki watajifunza kuandaa na kuoanisha viwango mabalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.

 

"Nchi nyingine za Afrika Mashariki hazipo vizuri kwenye biashara ya viungo ila kuna wenzetu wametoka Zanzibar wamebobea kwenye viungo na biashara ya viungo na baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara," amesema Dk Nyandoro.

 

Mshiriki kutoka Zanzibar Khamis Issa Mohamed ambaye anasafirisha bidhaa za viungo kutoka Zanzibar kwenda Ulaya amesema utaratibu wa kuoanisha viwango ndani ya nchi za Afrika Mashariki utaongeza tija kwenye bidhaa zao.

 

Mohamed amesema baada ya mafunzo hayo watajenga uelewa mzuri zaidi na kuwekwa utaratibu wa viwango vinavyolingana.

 

"Unapokuwa unasafirisha bidhaa inapaswa kuwa na viwango vinavyotakiwa na kuwa balozi kwani unapofanya vizuri unaitangaza nchi ila ukipeleka bidhaa isiyo na viwango unaitukanisha nchi yako,” amesema.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad