Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA inawataka wasafirishaji watoetiketi za kielektroniki kama kanuni zinavyoelekeza - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 4, 2021

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA inawataka wasafirishaji watoetiketi za kielektroniki kama kanuni zinavyoelekeza

 

 Pichani ni Mkurugenzi Mkuu LATRA Gilliard Ngewe (wa katikati) akiwa na Salum Pazzy ambaye ni Afisa Habari Mwandamizi  LATRA (Kulia kwa Mkurugenzi Mkuu) aliyevaa suti ya bluu, pamoja na Tadei Mwita ambaye ni Meneja Mradi wa Taketi Mtandao LATRA (kushoto kwa Mkurugenzi Mkuu)

***************************

Mamlaka inawaagiza wasafirishaji wote wa abiria kwa mabasi kuzingatia masharti ya leseni za usafirishaji na matakwa ya Kanuniza Leseni za Usafirishaji -Magari ya Abiria zilizotangazwa kwa tangazo na 76 kwenye gazeti la Serikali Februari 7, 2020 kama ifuatavyo;

Kanuni ya 4(2)(c); “Leseni ya kusafirisha abiria itatolewa kwa muombaji aliyesajiliwa kwenye mfumo wa tiketi za kielektroniki ulioidhinishwa na Mamlaka”.

Kanuni ya 24(b)(d); Msafirishaji mwenye leseni ya kusafirisha abiria wa masafa marefu ahakikishe anatoa tiketi za kielektroniki kwa abiria.” 

Mamlaka inawataka wasafirishaji watoetiketi za kielektroniki kama kanuni zinavyoelekeza. Kuanzia tarehe 6Januari, 2021 hakuna msafirishaji atakayeruhusiwa kusafirisha abiria bila kutoa tiketi za kielekroniki kwa abiria wotekatika njia zifuatazo;

i. Dar-es-Salaam Tanga 

ii.Tanga Arusha

iii. Dar es Salaam Lindi

iv. Dar es Salaam Mtwara

v. Dar es Salaam-Iringa  

vi. Dar es Salaam Njombe 

vii. Dar es Salaam Ruvuma 

viii. Dar es Salaam Mbeya

ix. Dar-es-Salaam-Tunduma  

x. Dar es Salaam Rukwa  

xi. Dar es Salaam Morogoro  

xii. Dar es Salaam Kilombero 

xiii. Dar es Salaam Ifakara

xiv. Dar es Salaam Malinyi

xv. Dar es Salaam Mahenge

Maelekezo ya utekelezaji wa agizo hili kwenye njia nyingine yatatolewa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad