HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 14 December 2020

VUTA NIKUVUTE 16 BORA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA.

  

 ***************************


 Na Piason Kayanda, Michuzi Tv

Droo ya 16 bora ya mashindano ya klabu bingwa barani ulaya imetangazwa rasmi mara baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi wiki iliyopita.

 Chelsea chini ya Frank Lampard wanakutana na Atletico Madrid ambao ni vinara wa ligi ya Uhispania Laliga, Liverpool wakiwa na majeraha ya wachezaji wake muhimu  wanakutana na RB Leipzig ambao waliwaondoa Manchester united kwa kuwafunga goli tatu kwa mbili.

Manchester City itasafiri kwenda Ujerumani katika hatua ya  kwanza ya michuano hiyo kumenyana na Wajerumani Borussia Monchengladbach,Pep Guardiola naManchester City yake wanatarajiwa kupigana  kwa nguvu kuweza kufika nusu fainali na Fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ambayo inaishiaga robo fainali tu.

Vita ambayo inasubiliwa kwa hamu ni vita ya Neymar dhidi ya mshikaji wake Lionel Messi ambapo  Barcelona watakipiga na Paris Saint-Germain amabapo mara ya mwisho timu hizi kukutana Barcelona waliwatoa Paris Saint- Germain kwa kipigo cha goli sita kwa moja.

Mechi nyingine ni Real Madrid watakao wakabili Atalanta,Sevilla atakipiga na Borrusia Dortmund, na Juventus wakutana na Porto ya huko nchini Ureno.

Huku mabigwa watetezi wa mashindano hayo ya klabu bingwa Barani Ulaya 2019/2020 Bayern Munich watachanga karata zao kwa mara nyingine tena  kuelekea kutetea ubingwa wao dhidi ya Lazio ya huku nchini Italia

Mzunguko wa 16 unatarajiwa kufanyika Februari na Machi mwaka  ujao wa 2021 ambapo tutaenda kushuhudia atae beba ubingwa kwa mwaka 2020/2021.

 


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad