RC KUNENGE AZINDUA RASMI ONYESHO LA CIRCUS MAMA AFRICA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 December 2020

RC KUNENGE AZINDUA RASMI ONYESHO LA CIRCUS MAMA AFRICA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelwa maonesho ya Circus Africa yanayoendelea katika Viwanja vya Jeshi Masaki.
Kunenge amefungua rasmi maonesho hayo ya Circus mama Africa na kutoa wito kwa wananchi kutembelea vivutio vya utalii.

Akizungumza baada ya kuzindua, Kunenge ameipongeza bodi ya utalii Tanzania (TTB) kwa kuendelea kuwa wabunifu Katika kuendeleza sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kuweka gharama nafuu ili kuwezesha kila mwananchi kumudu.

Tamasha hilo la Circus mama Africa linahusisha utalii wa michezo ya jukwaani na vivutio vya utalii.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa maonesho hayo yatadumu hadi Januari 10 2021, na yatahusisha michezo mbalimbali.

Amesema, watanzania wajitokeze kwa kwani hii ni michezo yao na inachezwa na watanzania wenyewe kwahiyo waende wenyewe kujionea vipaji halisi.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge (katikati) akifurahi pamoja  na Mkurugenzi Mwendeshaji Devotha Mdachi wakati wa uzinduzi wa aonesho ya Circus Mama Africa yanayoendelea katika Viwanja vya Jeshi Masaki.
Kikundi cha maonesho wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa maonesho ya Circus Mama Africa yaliyofanyika jana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad