DAWASA WAFIKISHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA NA SEGEREA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 December 2020

DAWASA WAFIKISHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA NA SEGEREA


Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuendeleza jitihada ili wananchi wapate huduma ya maji safi na salama.

Hayo ameyasema wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe- Pugu-Gongo la Mboto utakaohudumia wananchi wa Pugu hadi Tabata.

Katika ziara hiyo, Waziri Aweso alitembelea tanki la kuhifadhia maji na kushuhudia maji yakianza kuingia kwenye pamoja na kuzindua maji eneo la Kifuru.


Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini Dar es Salaam, Aweso amesema Dawasa wanafanya kazi nzuri sana chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanapata maji safi na salama.

Amesema, " DAWASA wametekeleza agizo la Rais wetu kwa kufikisha huduma ya Maji safi kwa wakazi wa Pugu ,Gongo la mboto, Majohe, Chanika,Ukonga na Segerea kabla ya Disemba 25 Mwaka huu, limetekelezwa,"


Aweso amesema, pia ameona maendeleo mazuri katika mradi huo naada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Tank kubwa la Maji linalopokea maji kutoka Kisarawe kwenda Pugu lenye uwezo wa kupokea na kusambaza Lita milioni 2.8 kwa siku lililojengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 6.9 lililoanza kupokea maji na kusambaza kwa wananchi.Mradi huo utahudumia wakazi wa Jimbo la Ukonga ikiwemo Pugu, Majohe, Gongo la mboto, Bangulo, Airwing, Kigogo, Chanika, Kinyamwezi, Banana, Segerea na Kifuru.


Aweso ameonyesha kufurahishwa na utekelezaji wa agizo hilo ndani ya muda mfupi na kuwataka DAWASA kuwekeza nguvu zaidi katika kuwaunganishia wananchi huduma hiyo ili kila mwananchi awe na huduma.


"Mradi huu tumeutekeleza Wizara kupitia DAWASA na ni faraja kwetu kuwa umekamilika ndani ya wakati na unaenda kuondoa shida yote ya Maji kwa maeneo yaliyopitiwa na mabomba hayo kuanzia Pugu hadi Kinyerezi"amesema Aweso


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge ametoa wito kwa wananchi kulipa bili za Maji ili kuiwezesha DAWASA kuendelea kupanua huduma kwani miradi mingi inayofanywa na Mamlaka hiyo inatumia fedha zake za ndani zitokananazo na makusanyo ya ankara za huduma ya Maji.


Aidha Kunenge amesema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wezi wa maji na wanaoharibu miundombinu ya Maji huku akiwaelekeza DAWASA kudhibiti tatizo la upotevu wa Maji.


Mradi wa Maji Kisarawe-Pugu - Gongo la mboto umetekelezwa na DAWASA baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji Kibamba- Kisarawe ulioleta uhitaji kwa wananchi wa maeneo hayo.

Jumla ya shilingi Bilioni 6.9 zimetumika hadi kukamilisha kwa mradi huo utakaonufaisha wakazi takribani 450,000.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifunga mita ya maji wakati akizindua huduma ya maji kwa wananchi wa Kifuru kupitia mradi wa maji wa Pugu - Gongo la Mboto ulioanza kufanya kazi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji Pugu. Waziri Aweso aliambatana na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Abubakar Kunenge, Mbunge wa Segerea Bonna Kamoli, Makamu Mwenyekiti wa Bodi na viongozi wengine

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo ya mradi wa maji Pugu-Gongo la Mboto kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kutembelea mradi huo ulioanza kutoa huduma kwa wananchi wa Gongo la Mboto hadi Kifuru,  Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge, Mbunge wa Segerea Bonna Kamoli pamoja na viongozi wengine wa serikali na DAWASA.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakipandisha juu ya tanki la maji kwa ajili ya kulikagua na kuona namba maji yalivyoanza kuingia.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiangalia namna maji yanavyoingia katika tanki la kuhifadhia maji la Pugu likipokea kutoka tanki la Kisarawe kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa  Pugu-Gongo la Mboto na kupata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kutembelea mradi huo ulioanza kutoa huduma kwa wananchi wa Gongo la Mboto hadi Kifuru,  Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge, Mbunge wa Segerea Bonna Kamoli pamoja na viongozi wengine wa serikali na DAWASA.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akimtwisha mama ndol ya maji kichwani baada ya kuzindua rasmi huduma ya maji Segerea mtaa wa Kifuru.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo ya mradi wa maji Pugu-Gongo la Mboto kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kutembelea mradi huo ulioanza kutoa huduma kwa wananchi wa Gongo la Mboto hadi Kifuru,  Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge, Mbunge wa Segerea Bonna Kamoli pamoja na viongozi wengine wa serikali na DAWASA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad