MWENYEKITI UVCCM AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA JIJINI DODOMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 31 December 2020

MWENYEKITI UVCCM AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA JIJINI DODOMA


 Dodoma

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Komred Kheri James Leo ameongoza Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na makada na wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika Mazishi ya aliekua Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM katika kipindi Cha Mwaka (2008-2017) na katibu wa idara ya Hamasa na Chipukizi Taifa.

Ndg Egla mwamotto amezikwa Leo nyumbani kwao Dodoma katika wilaya ya Chamwino kijiji cha Mpwayungi.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha Salam za pole komred kheri ametoa pole kwa familia, ndugu ,jamaa na marafiki kwa msiba huo na kuwaomba Kuwa na subira katika kipindi hiki.

Akitoa salamu za pole, amesema chama cha mapinduzi kimepata pigo kwa kuondokewa na kiongozi alietumikia chama na Jumuiya ya Umoja wa Vijana katika kipindi chote cha uhai wake kwa uaminifu na uadilifu.

Msiba huo umehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali pamoja na wajumbe wastaafu wa Baraza kuu la Umoja wa vijana wa CCM kuanzia mwaka 2008 hadi 2017.

”Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad