HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 31 December 2020

DC MTWARA ASISITIZA MPANGO WA KUWAKAMATA VIJANA WATAKAOSHINDWA KUJISHUGHULISHA NA KILIMO NA UVUAJI SAMAKI


 Na Mwaandishi Wetu Mtwara

MKUU wa Wilaya Mtwara Danstan Kyobya amesisitiza mpango wa kuwakamata vijana wote wilayani humu ambao watashindwa kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali pamoja na uvuaji wa samaki ifikapo Februari mwakani

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa alitoa maelekezo ya kuwakamata vijana pamoja na watu wengine ambao watashindwa kuanzisha mashamba yao na kuanza kulima mazao mbalimbali yakiwemo korosho ili kujipatia kipato cha kuboresha maish yao.

Alisema kwa yeyote ambaye atashindwa kufanya hivyo ifikapo Januari mwakani atakamatwa na kutozwa faini ya shilingi 50,000 na kulazimika kuanzisha mashamba na kulima kwa nguvu.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa ameanzisha kampeni, ondoa pori ongeza uzalishaji, tumetoa mda wa mwei mmoja, inapofika tarehe moja Februari hatutaki kuona kijana yeyote anazurura, tunakata kila kijana either anavua samaki au ana shamba lake la kulima, na kama utakuwa huna kazi ujue tutakukamta kwa uzururaji na kwenda kwenye nyumba za serikali ambazo hazijai,” amesema.

Amewataka vijana wote wa kike na kiume Wilayani humu kufaya maamuzi sasa hivi na kuamua endapo waende kuvua samaki huku akisema kuwa soko la samaki lipo na wanunuzi wapo na kama ni kwenda kulima mashamba yapo.

“Kila kijana ahakikishe kufikia tarehe moja mwezi wa pili, una shamba lako lenye hekari zako za kutosha, unalima korosho, ufuta, mbaazi, maharage, mahindi, viazi,  au unashinda baharini unavua samaki,” amesema.

Kyobya amewaomba wenye viti wa kata pamoja na madiwani kuhakikisha mpango huo unasimamiwa huku akisisitiza kwamba maelekezo hayo hayarudi nyuma na kwamba ikifika tarehe mbili mwezi wa pili mwakani wataanza kukamata yule ambaye atakuwa anazurura atatozwa faini ya shilingi 50,000 na kwamba ambaye hatakuwa na faini hiyo atawekwa ndani.

Amewata wenye mashamba pori kuyafyeka na kuanza kuayalima na kama hawawezi wapatiwe watu wengine walima au litachukuliwa na serikali kwa kuwa wenye mashamba hayo watakuwa wameshindwa kuyaendeleza.

“Kama mwenye pori kashindwa kuendeleza sheria zipo wazi mnalichukua sheria, tunataka tubadlishe halmashauri zetu kwa kuhakikisha shughuli za kimaendeleo zinafanyika,” amesema.

Kyobya amesema hayo wakati akizindua soko la samaki katika kata ya Msangamkuu Wilaya ya Mtwara Vijijini. Amewataka vijana, pamoja na akina mama kutumia fursa za biashara katika soko hilo kujiongezea kipato  cha kuinua mapato ya halmshauri ya wilaya hiyo.

Soko hili ambalo limejengwa kwa mapato ya ndani na nguvu za wananchi limegharim kiasi cha shilingi milioni 78.5 huku wananchi wakichangia kiasi cha shilingi million 9.5.

Katika hatua  nyingine, Kyobya amewataka watendaji kuhakikisha soko hilo linakuwa na ‘masterplan’ ya jinsi soko hilo litapokuwa litakapomalizika na pia kuhakikisha miundombinu rafiki inawekwa zikiwemo barabara za kuingia na kutoka sokoni.Mkuu wa Wilaya akizindua Soko la Msangamkuu lililoko kata ya Msangamkuu Mtwara DC. Soko hilo lenye thamani ya shilingi 78.5 milioni limejengwa Kwa kutumia mapato ya ndani pamoja na Nguvu ya wananchi ambao walichangia kiasi cha shilingi milioni 9.5.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad