Mwenyekiti
TLB Manispaa ya Iringa David Mgimwa akizungumza na waandishi wa habari
juu la ombi lao la kupewa elimu ya magonjwa ya milipuko.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA cha watu wenye ulemavu wa macho TLB Mkoani Iringa kimeeleza
kuwapo kwa hofu juu ya wanachama wake kuambukizwa magonjwa ya milipuko
kutokana na kundi hilo kutopatiwa elimu ya kujikinga magonjwa hayo.
Mwenyekiti
wa TLB mkoani Iringa Huruma Maketa alisema tangu kuibuka kwa maambukizi
ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19 nchini kundi
la walemavu walikuwa wanahitaji elimu maalum kwa ajili ya kuhakikisha
wanajikinga na ugonjwa huo kwa kuwa kundi hilo halijawahi kukumbukwa na
walikuwa hatarini zaidi kupata maambukizi hayo.
Maketa alisema
kuwa kundi hilo limekuwa likisahaulika mara kwa mara kupata elimu ya
magonjwa ya milipuko kuliko makundi mengine yote hivyo serikali na wadau
wengine wanapaswa kujitolea kutoa elimu kwa walemavu hao.
Alisema
kuwa kunapotokea milipuko ya magonjwa kama kipindupindu,homa ya matumbo
na Corana wanakuwa hawapata elimu hiyo kwa wakati na kushindwa kupata
mbinu sahihi za kujikinga na magonjwa hayo.
Maketa alisema kuwa
watu wenye ulemavu hawaoni mambo yanayoendelea kutokana wao kuweza
kusikia tu hivyo ikitolewa elimu mara kwa mara itasaidia kundi hilo
kuepukana kukumbwa na magonjwa hayo ya milipuko.
Aidha kwa
upande wake Mwenyekiti TLB Manispaa ya Iringa David Mgimwa alisema kuwa
walikuwa wanakukumbana na unyanyapaa kutoka kwa watu waliokuwa
wakiwasaidia kuwaongoza barabarani kukataa kuwashika mkono wakati wa
kipindi cha Corona kwa hofu ya kupata maambukizi hayo.
Mgimwa
alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa watu wenye
ulemavu ili kuwasaidia kuepukana na kujikinga na magonjwa ya milipuko
ambayo yanayokuwa yanatokea mara kwa mara bila watu wenye ulemavu kujua
nini kinaendelea wala kutokujua namna ya kujikinga na magonjwa hayo.
Mgimwa
aliwaomba wananchi kuendelea kuwasaidia na kutoa elimu kwa watu wenye
ulemavu wa macho pale yanapotokea magonjwa ya milipuko ili kuwasaidia
walemavu hao kujikinga kupata magonjwa hayo ya milipuko.
Lakini
pia jamii imeshauriwa kuwashika mkono watu wenye ulemavu wa macho hasa
katika kipindi cha mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vya Corona COVID
19 kwani wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na
hali zao.
Akizungumza na mwandishi wetu mganga mkuu wa Manispaa
ya Iringa, Dk. Jesca Leba alisema kwamba kutokana na hali walizonazo
walemavu wa macho kuna umuhimu mkubwa wa jamii kuwa nao sambamba kwani
wako katika hali ya hatari zaidi kutokana na hali zao za kutokuona hivyo
elimu na kuwaongoza namna ya kunawa mikono itasaidia katika mapambano
hayo.
Alisema kuwa kama manispaa wametoa mafunzo kwa walemavu na
wataendelea kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya walemavu kwa ajili
ya kushikwa mkono kwani changamoto kubwa kwenye vyombo vya kunawia
mikono wanashindwa kuelewa mahali ilipo.
“Kwa kweli kuna
changamoto kubwa kwa walemavu na ndio maana tumeamua kufanya mafunzo
kwao tena maalum kwa kundi la walemavu wa macho na tutafanya mafunzo
haya kwa makundi yote kwa sababu watu wanaohitaji kushikwa mikono katika
kuwaongoza” alisema
Aidha katika mafunzo hayo, Dk Leba
aliwataka walemavu wa macho kuepuka kushika macho, pua na mdomo kwa
mikono isiyo safi kwa sababu mikono ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi
na kuzingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au
kupiga chafya.
Alisema kuwa endapo binaamu atahisi kuwa na mafua
makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kupata
msaada wa kitaalamu na kuepuka kuwa sehemu yenye msongamano kama vyombo
vya usafiri, maduka na maeneo yenye mgandamizo wa hewa.
Monday, November 9, 2020
WATU WENYE ULEMAVU WA MACHO IRINGA WAOMBA KUPEWA ELIMU YA MAGONJWA YA MILIPUKO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment