HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 9, 2020

TAHADHARI YA MVUA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa Inatarajiwa kunyesha kwa siku tatu mfululizo  kuanzia leo Jumapili Novemba 8,  2020.

Katika Utabiri wao, TMA  imesema mvua  zinatarajiwa kunyesha katikati mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro,Tanga, visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Zinatarajiwa kuanza leo hadi Novemba 10, 2020 na  kwamba inatarajiwa maeneo hayo yatakuwa yenye tahadhali kubwa hususani  leo na kesho ambapo vipindi vikubwa vya mvua vinatarajiwa kujitokeza

Aidha TMA wamesema, athari mbali mbali zinaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na mafuriko kwenye makazi ya watu, baadhi ya barabara kufungwa na shughuli za kiuchumi kusimama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad