Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHIRIKA
la Childbirth Survival International(CSI) limesema linatoa pongezi na
kuunga mkono jitihada ambazo zinafanywa na Taasisi ya Dorris
Mollel ambayo imejikita kusaidia watoto njiti ikiwa pamoja na
kuhakikisha wanapata malezi yanayostahili pamoja na kufuatilia malezi na
makuzi yao.
Akizungumza
wakati wa tukio lililoandaliwa na Dorris Mollel Foundation la kutoa
huduma za afya kwa watoto njiti lililofanyika Don Bosco jijini Dar es
Salaam, Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester Mpanda amesema
kwamba shirika lao linajihusisha na afya ya mama na mtoto hasa katika
kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na mtoto wakati wa
kujifungua.
"Hivyo
tuko hapa kwasababu ya kusadia kazi zinazofanya na Dorris Foundation
kwani ni kitu ambacho sisi pia tunakifanya kwa njia moja au nyingine
maana tumejikita katika kuhakikisha mama na mtoto wanakuwa salama.
"Hivyo
tumefurahishwa na kazi yake na tunachokifanya CSI ni kumuunga mkono na
kumtia nguvu kwa kazi anayofanya ili aweze kufikia jamii kubwa,"amesema
Ester Mpanda.
Kuhusu
ujumbe wa CSI kuelekea siku ya mtoto njiti Novemba 17, 2020, Ester
Mpanda amesema wanaiomba jamii hasa inayoishi na mtoto Njiti kuhakikisha
anafuatilia vema na kufuata ushauri wa madaktari kuhakikisha mtoto
anakuwa salama na tukio lililoandaliwa na Dorris Foundation la kuandaa
madaktari bingwa kwa ajili ya kuangalia maedeleo ya watoto njiti linatoa
nafasi kwa wazazi kujua maendeleo ya watoto.
"Tukio
hili ambalo limefanyika siku ya leo ni muhimu, jamii isipuuze kwani
inatoa nafasi ya mzazi au mlezi kujua hali za watoto wao, kwani mtoto
njiti maana yake amezaliwa kabla ya muda , hivyo afya mara nyingi
inakuwa sio nzuri.
"Hivyo
wanapokuja kujua hapa inakuwa rahisi kujua hali za watoto kama kuna
viashiria vya ulemavu au wanaendelea vizuri, jamii inaposikia vitu vya
aina hiyo waitikie mwito kwani vinafaida kwa mtoto na wazazi kwa
ujumla,"amesema
Alipoulizwa
kuhusu jitihadaza za CSI katika kusaidiana na Serikali na wadau wengine
kupunguza vifo vya mama na mtoto, Mpanda amesema kwa sasa hivi hali ni
nzuri na kwamba hata hotuba ya Rais John Magufuli imeeleza jinsi vifo
vya mama na mtoto ambavyo vimepungua.
"Vifo
vimepungua sana na kusababu nyingi ambazo zimesababisha, mbali ya elimu
ambazo wadau tunatoa tukiwemo sisi CSI, lakini Serikali imefanya kazi
kubwa kuboresha miundombinu, kuna zahanati, vituo vingi vya afya na
hospitali.
CSI
tunashirikiana na Serikali kwa mambo mengi tunayofanya na kwa hakika
imefanikiwa kupunguza hivyo hivyo.Mkakati wetu i kuendelea kusehemu ya
timu ya Serikali na kuhakikisha tunaendelea kutoa elimu ya uzazi salama
kuanzia ngazi ya chini kwa makundi ya vijana mpaka kwa mama wajawazito
na wazazazi kwa ujumla,"amesema.
Alipoulizwa
nini ambacho CSI wanafanya katika kupunguza vifo vya mama na mtoto ,
Mpanda amesema wamekuwa wakitoa elimu ya uzazi salama , wamekuwa
wakisaidia vifaa vya kuzalia , kutoa elimu kwa jamii kutambua viashiria
vya hatarishi, wanazo programu maalum kwa ajili ya wasichana
inayozungumzia masuala ya uzazi na viashiria hatari vya uzazi ambavyo
wakiviona vile wanajua wanatakiwa kuanza kliniki mapema.
"Kwa
hiyo tumekuwa tukitoa elimu kwa ujumla kuhusu masuala ya uzazi na hasa
uzazi salama kuanzia mimba ikiwa changa hadi pale inapofika miezi tisa
na hiyo ndio imekuwa kazi ya CSI kwa muda mrefu ma mpaka sasa.
"Tumefika
katika mikoa 10 nchini Tanzania na tunaendelea kufanya. Pia sio hapa tu
bali tupo nchini Rwanda, Kenya, Somalia, Uganda na Marekani ambako
ndiko kuna makao makuu yetu.Hivyo hata ukiangalia mitandao yetu ya
kijamii ya Instagramu, facebook, utaona kazi ambazo CSI
tunafanya,"amesema Mpanda.
Madakatari
kutoka hospitali mbalimbali za Jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi
ya kuwachunguza watoto Njiti kwa ajili a kujua afya zao ili kuwaepusha
na magonjwa mbalimbali yanayoweza kuwakabili wakati wa zoezi la kutoa huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Programu za Vijana kutoka CSI, Ester Mpanda, timu ya Shirika la
Childbirth Survival International(CSI) pamoja na timu ya Dorris Mollel
Foundation wakiwafanyia usajili mama na mtoto waliofika kwa ajili ya
watoto Njiti kufanyiwa uchunguzi na madaktari kutoka hospitali ya
Muhimbili, Aga Khan na kuandaliwa na Dorris Mollel Foundation
iliyofanyika Don Bosco jijini Dar es Salaam
Watoto Njiti wakisubilia kupewa huduma na Madakatari kutoka Muhimbili na Aga Khan wakati wa zoezi la kutoa huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.Meneja
wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester Mpanda(kushoto) akizungumza na
mmoja wa mama aliyejifungua mtoto Njiti aliyefika katika zoezi la kutoa huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Dorris Mollel Foundation, Dorris Mollel(wa pili kushoto) akiwa
kwenye picha ya pamoja na timu ya Shirika la Childbirth Survival
International(CSI) waliofika kwa ajili ya kutoa mchango kwa Dorris
Mollel Foundation.
No comments:
Post a Comment