BENKI YA NMB YATOA MISAADA KATIKA SEKTA YA AFYA NA ELIMU YENYE JUMLA YA SHILINGI MILIONI 12.5/= WILAYA YA KILWA MKOANI LINDI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 24, 2020

BENKI YA NMB YATOA MISAADA KATIKA SEKTA YA AFYA NA ELIMU YENYE JUMLA YA SHILINGI MILIONI 12.5/= WILAYA YA KILWA MKOANI LINDI

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa - Renatus Mchau akipokea msaada wa madawati 100 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini - Janeth Shango .Katikati ni Nelly Masisi – Meneja wa NMB Tawi la Kilwa. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wazazi pamoja na wanafunzi wa Shule hiyo .

========   =========   ==========

Benki ya NMB imetoa misaada kwa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi katika sekta ya afya na elimu yenye jumla ya shilingi milioni 12.5 

Akikabidhi misaada hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa - Renatus Mchauru, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini - Janeth Shango, alisema wakati anapata matibabu katika kituo cha afya Masoko, alibaini mapugufu yaliyokuwepo katika kituo hicho na alipozungumza na utawala walimweleza tatizo na akawashauri waandike barua ya kujieleza, kitu ambacho walifanya.

Alisema Benki ya NMB imekarabati jengo la Baba, Mama na Mtoto kwa kuweka paa jipya, kupaka rangi na kuweka michoro ambayo inaleta taswira njema kwa wadau wanaofuata tiba. Alisema Benki hiyo inaona fahari kusaidia eneo hilo ili liwe rafiki kwa wahitaji.Alisema kazi ya kukarabati jengo hilo la hospitali katika kituo cha afya Masoko uligharimu Sh milioni 2.5.

Naye Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, John Nkuba alishukuru Benki ya NMB kwa msaada wake na kusema kwamba mazingira ya matibabu sasa baada ya ukarabati huo yako bora zaidi.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa- Renatus Mchauru pamoja na kushukuru kwa misaada hiyo, aliwataka watumishi kuhakikisha wanatoa huduma nzuri na bora zaidi kulingana na uzuri wa majengo yaliyopo sasa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati katika shule ya msingi ya Msingi Kipindimbi, Shango alisema wametoa madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wapya wa shule hiyo.

Shule hiyo iliyokuwa na madawati 100 ilizidiwa baada ya wanafunzi kuongezeka kufuatia maafa ya mafuriko yaliyokumba shule na makazi katika kata ya Njinjo mwanzoni mwa mwaka huu. Shule hizo ni pamoja na Njinjo na Ndende.

Maafa hayo yaliyokumba watu zaidi ya 6,804 katika kata ya Njinjo yalisababisha Shule ya Kipindimbi wanafunzi wake kuongezeka kutoka watoto 400 hadi 909 na kusababisha upungufu wa madawati zaidi ya 100.

Katika hafla zote mbili Shango alishauri wazazi kuanza mapema kuwafunza watoto wao kuweka akiba kwa kuwafungulia akaunti watoto wao ili waweze kuja kujisaidia siku za baadae.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Bahati alisema pamoja na kusaidiwa madawati hayo , shule hiyo bado inakabiliwa na tatizo la matundu ya choo kwa wanafunzi na walimu na pia nyumba za walimu.

Wanafunzi wa shule hiyo Khalid Salim na Neema Ali waliishukuru Benki ya NMB kwa kuwasaidia madawati hayo na kuwataka wawasaidie pia matundu ya choo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad