Mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Dokta Jescar Leba amewataka wakinamama wanaojifungua kufuata maelekezo ya wataalamu ikiwemo kutowaongezea chakula chochote watoto pindi wanapozaliwa hadi kufikia umri wa miezi sita kwa lengo la kulinda afya zao.
Dokta
Leba ametoa rai hiyo kwenye shughuli ya wakina mama wenye watoto chini
ya miezi 6 ijulikanayo kama “Mother Meetup” iliyoandaliwa na na mradi wa
USAID TULONGE AFYA kupitia jukwaa la NAWEZA kwa lengo la kuwakumbusha
wakinamama hao juu ya malezi bora ya watoto ambapo amesema watoto
wanaozaliwa hawapaswi kuongezewa chakula chochote kwakuwa nyongeza hiyo
ya chakula inaweza kuathiri afya na ukuaji wao kimwili na kiakili.
Aidha
Dokta leba ameongeza kuwa zipo mila na desturi mbaya zilikuwa
zinaathiri kampeni hiyo lakini kwa juhudi za serikali na wadau wa
maendeleo, jamii imeelewa umuhimu wa unyonyeshaji maziwa ya mama pekee
na kuanza kufuata utaratibu huo na kuongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu
walizonazo kwasasa unyonyeshaji bila nyongeza ya chakula kwa miezi sita
ni karibu asilimia mia moja
“Tulikuwa
na changamoto ya mila na desturi katika eneo hili ambapo wazazi
walikuwa wakishinikizwa na wanafamilia mfanobibi au majirani kwamba
mtoto akilia anapaswa kupewa uji au hata maji kwa madai kuwa maziwa ya
mama pekee hayatoshi lakini kwa sasa wengi wamekwishaelewa na
utekelezaji ni karibu asilimia mia moja”. Aliongeza Dokta Leba
Baadhi
ya wakinamama hao wametoa ushuhuda na kueleza kuwa changamoto ya mila
na desturi ilikuwa kikwazo kutokana na jamii inayowazunguka kulazimisha
watoto kupewa nyongeza ya chakula ndani ya muda mfupi wa kuzaliwa kwa
madai kuwa maziwa yam am hayawezi kumtosheleza
“Mimi
nilipojifungua ndani ya kipindi cha wiki mbili mtoto wangu wa kwanza
alikuwa analia sana ndipo nikaambiwa nimuongezee chakula kwa madai kuwa
maziwa yangu yalikuwa hayatoshi. Lakini nilikataa na kuendelea
kumnyonyesha mwanagu mpaka alipofikisha miezi sita ndipo nikaanza
kumuongezea vyakula na mpaka sasa ana afya njema”. alisema bi. Theresia
Joseph ambaye ni mama wa watoto wawili
Sezaria
Andrew ni yeye ni mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wa manispaa ya
Iringa alisema pamoja na hamasa iliyofanywa na serikali katika
kuhakikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi
sita unazingatiwa, mchango wa wadau wa maendeleo kupitia miradi
mbalimbali kama mradi wa USAID Tulonge Afya si wakubezwa katika
mafanikio yaliyofikiwa kwenye kampeni hiyo.
“Tunawashukuru
wadau wetu USAID TULONGE AFYA kwani wamekuwa kiungo cha mabadiliko ya
tabia ndani ya jamii, ,tunawaomba waendelee kutuunga mkono ili tuendelee
kumpambania mtoto wa kitanzania. Watoto wanaoanzishiwa chakula kabla ya
miezi sita ya kuzaliwa wengi husumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo
magonjwa ya tumbo kutokana na utumbo kutokuwa na uwezo wa kuchakata
chakula” alisema dokta Sezarina Andrew.
Mradi
wa USAID Tulonge Afya ni mradi miaka mitano unatekelezwa na Serikali ya
Tanzania kwa kushirikiana na shirika la FHI360 na wadau wengine
wakiwamo mashirika ya TCDC na TMARC chini ya ufadhili wa shirika la
kimarekani lijulikanalo kama USAID. Mradi huu unatekelezwa hapa nchini
katika Wilaya 29 kwenye mikoa 12. Kwa upande wa mkoa wa Iringa mradi
unatekelezwa katika wilaya tattu ambazo ni Iringa Manispaa, Mufindi DC
na Kilolo DC.
Mmoja
wa akina mama waliohudhuria kongamano la onyonyeshaji linalojulikana
kama Mother Meet Up event lililoandaliwa na USAID TULONGE AFYA mjini
Iringa Pendo Muhongole akifuatilia kwa makini maelezo ya mgeni rasimi
kwenye kongamano hilo.
Mgeni
rasmi wa kongamano la unyonyeshaji linalojulikana kama Mother Meer Up
event lililoandaliwa na USAID TULONGE AFYA mjini Iringa Dkt Jescar Leba
(mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa) akiongea na akinamama
wakati wa kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment