Cristian Ronaldo aweka kambani goli la 101 katika timu ya taifa ya Ureno - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 9, 2020

Cristian Ronaldo aweka kambani goli la 101 katika timu ya taifa ya Ureno

Na Lusajo Frank, Dsj
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Ureno, Cristian Ronaldo Dos Santos Aveiro {Cr 7} amefanikiwa kufikisha magoli 101 katika timu ya taifa.

Cristian Ronaldo aliweka kambani magoli mawili katika mchezo dhidi ya Sweden uliopigwa katika dimba la Friends Arena mjini Solna Sweden.

Ureno iliibuka na ushindi wa magoli wa mawili kwa sifuri dhidi ya Sweden, katika michuano ya ligi ya timu za taifa  (UEFA national league).

Ronaldo anakuwa mchezaji wa pili kufunga zaidi ya mabao 101 katika michezo 165 ya timu taifa na mchezaji namba moja ulaya, huku rekodi hiyo ikiwa bado inashikiliwa na Ali Daei, raia wa Iran akiwa na magoli 109.

Cristian Ronaldo anahitaji magoli 8 kuvunja rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwenye mechi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad