Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano aliyemwakilisha Mkuu wa
Wilaya ya Chemba, Simon Chacha akizungumza alipokuwa akifunga
Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Shule ya Msingi Chemba, wilayani hapa.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (kulia)
akipata maelezo kwenye Banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET)
alipotembelea mabanda ya taasisi wanachama wa mtandao huo, kwenye hafla
ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini yaliyofanyika kwenye
viwanja vya Shule ya Msingi Chemba. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Mtandao wa Elimu (TEN/MET), Dk. John Kalage pamoja na Mratibu wa Taifa
wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (kulia)
akipata maelezo ndani ya Banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET)
alipotembelea mabanda ya taasisi wanachama wa mtandao huo, kwenye kilele
cha Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja
vya Shule ya Msingi Chemba. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa
Elimu (TEN/MET), Dk. John Kalage pamoja na Mratibu wa Taifa wa TENMET,
Bw. Ochola Wayoga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu (TEN/MET), Dk. John Kalage
(katikati) akihutubia kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la
Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Kushoto ni Mgeni rasmi na Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano
pamoja na Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (kulia)
wakifuatilia.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (kulia)
akipata maelezo ndani ya Banda la Uwezo Tanzania namna wanavyotekeleza
miradi mbalimbali alipotembelea mabanda ya taasisi wanachama wa mtandao
huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini yaliyofanyika
kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (wa pili
kulia) akipata maelezo ndani ya Banda la Uwezo Tanzania namna
wanavyotekeleza miradi mbalimbali alipotembelea mabanda ya taasisi
wanachama wa mtandao huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu
nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (wa pili
kushoto) akikabidhiwa fomu y kujiunga na marafiki wa elimu ndani ya
Banda la Haki Elimu alipotembelea mabanda ya taasisi wanachama wa
mtandao huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba. Anaye mkabidhi
ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu (TEN/MET), Dk. John Kalage, ambaye pia
ni Mkurugenzi wa HakiElimu.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (kulia)
akipata maelezo ndani ya Banda la HakiElimu alipotembelea mabanda ya
taasisi wanachama wa mtandao huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma
la Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (kulia)
akipata maelezo kwenye mabanda mbalimbali alipotembelea mabanda ya
taasisi wanachama wa mtandao huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma
la Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (wa pili
kulia) akipata maelezo ndani ya Banda la Shule Direct namna
wanavyosaidia sekta ya elimu alipotembelea mabanda ya taasisi wanachama
wa mtandao huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (wa pili
kulia) akipata maelezo kwenye mabanda mbalimbali alipotembelea mabanda
ya taasisi wanachama wa mtandao huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya
Juma la Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi
Chemba.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (kulia)
akipata maelezo kwenye Banda la CAMFED alipotembelea mabanda ya taasisi
wanachama wa mtandao huo, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu
nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Meneja Miradi wa CAMFED, Anna Sawaki (mwenye kipaza sauti)
akimwelezea Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano
(kulia) alipotembelea Banda la CAMFED, kwenye kilele cha Maadhimisho ya
Juma la Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi
Chemba.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano akimkabidhi
zawadi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Chemba aliyefanya vizuri
kwenye katika mitihani kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu
nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Baadhi ya wanafunzi wa msingi na sekondari wakiangali video ya
mafunzo ndani ya Banda la Uwezo Tanzania, kwenye hafla ya kilele cha
Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini yaliyofanyika wilayani Chemba.
Na Mwandishi Wetu, Chemba
SERIKALI wilayani Chemba imeahidi kuzifanyia kazi changamoto za elimu
ya msingi na sekondari zilizoibuliwa katika mijadala ya Maadhimisho ya
Juma la Elimu lililofanyika wilayani hapo kwa kukutanisha wadau anuai wa
elimu nchini.
Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha
katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi
Stephano akimwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa Maadhimisho ya Juma
la Elimu nchini zilizofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba
mjini hapa.
Alisema Serikali inaushukuru Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) na
wadau wote kwa kuleshughuli za Maadhimisho ya Juma la Elimu wilayani
Chemba kwani uamuzi huo ni kuipa kipaumbele wilaya hiyo ili iweze
kufanya vizuri zaidi katika sekta ya elimu. Aliongeza kuwa jitihada
zinazozifanywa na Serikali kuinua elimu lazima ziungwe mkono na wazazi
wa eneo husika, wadau wa elimu na wananchi kwa ujumla ili ziweze kuleta
mafanikio.
"...Serikali haiwezi kufanya mambo haya peke yake bila wazazi na
wadau wa elimu kuunga mkono, na hili lipo wazi hata ukiangalia maeneo
mengine ambayo nguvu za wananchi na Serikali zikiungana sekta ya elimu
inafanya vizuri kuanzia miundombinu na hata ufaulu wa wanafunzi,"
alisema Bi. Stephano akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chemba.
Aidha alisema Serikali ya Wilaya inaahidi kuzifanyia kazi changamoto
zote zilizoibuliwa katika mijadala ya elimu katika juma la maadhimisho
na kuwaomba wazazi na wananchi waeneo husika kushirikiana na viongozi
kutatua changamoto hizo.
Akizungumza awali, Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu (TEN/MET), Dk. John
Kalage alisema Maadhimisho ya juma la Elimu wilayani Chemba, yamepata
mafanikio makubwa kutokana na mapokezi na ushirikiano mzuri wa viongozi
na watendaji wa serikali, wanajamii, walimu na wanafunzi.
Alibainisha kuwa, muitikio huo wa jamii unadhihirika pia katika
baadhi ya miradi inayotekelezwa na jamii za shule husika zikiwemo,
Kushiriki ujenzi wa miundombinu ya shule yakiwemo Mabweni, Vyumba vya
madarasa, nyumba za walimu, ujenzi wa Vyoo, na kusaidia jitihada za
upatikanaji wa maji na hata kuchangia huduma za vyakula kwa wanafunzi
wakiwa shuleni, Ingawa bado kuna changamoto katika suala la ushiriki wa
wananchi kukamilisha miradi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la
Elimu nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chemba.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chemba wakitoa burudani kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu.
Alizitaja baadhi ya changamoto zilizoibuka katika mijadala kuwa ni
upungufu wa maabara na vifaa vya maabara, upungufu wa vitabu, walimu na
nyumba za walimu, upungufu wa matundu ya vyoo, uhaba wa maji safi na
salama kwa wanafunzi na walimu, upungufu wa madawati, pamoja na ukosefu
wa nishati ya umeme.
"...Wanafunzi wengi bado wanatembea umbali mrefu kufika shuleni na
kurejea nyumbani, ambapo baadhi yao wanatembea kilomita takribani sita
mpaka kumi na tano kwa siku. Changamoto hii imejidhihirisha zaidi kwa
wanafunzi wa shule za sekondari. Hali hiyo huwafanya wanafunzi kuchelewa
shuleni, kuchoka na kukosa muda wa kujisomea na kusababisha utoro wa
rejareja."
Hata hivyo, Dk. Kalage alisema mtandao unapendekeza uwajibikaji wa
pamoja katika kuifikia elimu bora na jumuishi; hivyo ipo haja ya
Serikali, jamii na Wadau kuongeza jitihada zaidi za kujenga miundombinu
ya kutosha kwa wanafunzi na walimu, ilhali jamii iendelee kuhamasishwa
kuithamini elimu na kuchangia nguvu kazi na raslimali katika kuboresha
elimu na kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (kulia) akiwapa
zawadi Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chemba walipokuwa wakitoa burudani
kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu.
Mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Goima, Bi. Rhobi Stephano (wa kwanza
kushoto) aliyemwakilisha DC Chemba, akiwasili kwenye kilele cha
Maadhimisho ya Juma la Elimu.
No comments:
Post a Comment