HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 31, 2020

KAYA 1320 ZAOMBA KUJITOA TASAF WARIDHIKA NA UCHUMI WAO

 

Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Nchini Satanslaus Mwamanga akizingumza  katika kikao cha kazi cha kujengea uwezo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF (PSSN)
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizingumza  katika kikao cha kazi cha kujengea uwezo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF (PSSN)
Mwenyekiti wa muda katika kikao hicho kwa kuchaguliwa na wajumbe ndugu Bahati Nyakiraria akitoa neno la shukrani mara baada ya mgeni rasmi kufungua kikao hicho leo katika ukumbi wa Arusha DC leo augusti 2020-01 septemba 2020
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho cha kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF (PSSN II)
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho cha kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF (PSSN II)

======  ======  =====

Na Vero Ignatus,Arusha

Kaya 1320 zimetajwa kuomba kujiondoa kwenye mpango wa kuhudumia Kaya masikini TASAF katika mkoa wa Arusha wakati serikali ikipanga kutekeleza mpango huo kipindi cha pili awamu ya Tatu kutokana na kujikwamua kiuchumi baada ya kuwezeshwa na TASAF.

Idadi ya Kaya hizo kujitoa katika mpango huo umeelezwa na Mkurugenzi wa TASAF Ladislaus Mwamanga wakati wa Kika kazi Cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mpango huo kipindi Cha ili awamu ya Tatu unaotarajiwa kuanza Mara badaa ya Uchaguzi Mkuu kupita 

Akizungumza kwenye kikao kazi hicho Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga alisema kuwa dhamira kubwa yaa Tasaf ni pamoja na  kuupunguza umasikini kwa kuzingatia uwazi uwajibikaji,na ushirikishwaji wa katika kuleta Maendeleo.

Mwamanga amesema kuwa mpango huo umewezesha utoaji ajira za muda katika halmashauri 42 Tanzania bara na Tanzania zanzibar ambapo jumla ya miradi 7,775 imetekelezwa katika vijiji,mitaa na shehia 1,928 na kufikia jumla ya walengwa 253,117 kwa kupata ajira za muda 

Utekelezaji wa TASAF awamu ya kwanza jumla ya miradi 1,704 ilitekelezwa na jamii yenye thamani ya shilingi Bilioni 72 kwenye halmashauri 40 Tanzania bara na Zanzibar  ambapo miradi 1,338 ya huduma za jamii ,miradi 61 ya makundi maalum na miradi 305 kutoa huduma za muda

 Kwa awamu ya pili jumla ya miradi 12,347 yenye thamani ya shilingi bilioni 430 ilitekelezwa na jamii katika halmashauri 126,miradi 4,297 ya huduma ya jamii kutoka sekta zote,miradi 6,260 makundi maalum,miradi 1,790 ya kutoa ajira za muda yenye  walengwa  152,458,vikundi 2,778 vya kuweka akiba na kuwekeza nyenye wanachama 27,800, ambapo utekelezaji wa miradi hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa haswa katika sekta za elimu,Afya,Maji na barabara za vijijini

Katika awamu ya tatu jumla ya kaya milioni 1.3 zilitambuliwa katika halmashauri zote za Tanzania bara na Zanzibar (Unguja na Pemba)Jumla ya kaya maskini milioni 1.1 zenye watu takribani milioni 5 ziliandikishwa na asilimia 52 ya walengwa ni wanawake ,mpango huo ulitekelezwa katika jumla ya vijiji,mitaa na shehia 9,986 ambapo jumla ya shilingi bilioni 968.7 zimetumika kwa walengwa wa mpango mpaka februari 2020
Akieleza chagamoto ambazo wanakutana nazo uwepo wa vijiji ,mitaa na shehia nyingi zenye kaya maskini ambazo hazijafikiwa kwasababu ya upungufu wa rasilimali fedha 30%ya vijiji ,mitaa na shehia,ukosefu wa fedha kwaajili ya kutekeleza miradi ya jamii kuboresha miundombinu,kuwepo kwa kaya ambazo siyo maskini kwenye mpango 

Akifungua kikao kazi hicho mgeni wa heshima ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amepongeza hatua ya mfuko huo wa kuhudumia kaya masikini nchini TASAF kuanza mpango kwa kushirikisha waandishi wa habari kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika kufikisha ujumbe kwa hadhira husika.

hata hivyo amewashauri waandishi wa habari kuzingatia uweledi wakati wa kuripoti hatua mbalimbali za mpango huo ili kutojenga taharuki ya kiuelewa kwa jamii na walengwa wenyewe lakini pia na kuepuka upotoshwaji.
Hata hivyo serikali ilianzisha Mfumo wa Maendeleo kwa Jamii (TASAF) mwaka 2000 kwa madhumuni ya kusaidiana na vyombo vingine vya serikali kupunguza umaskini,ambapo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali katika ngazi za jamii kwa lengo la kutoa huduma za kijamii katika sekta zote kwa kuzingatia mahitaji halisi au kero za wananchi na imetekelezwa kwa awamu tatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad