HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 4, 2020

BENKI YA MAENDELEO TIB YAENDELEA KUHAMASISHA UWEKEZAJI

Na Mwandishi wetu.
Benki ya Maendeleo TIB imeendelea kuhamasisha shughuli za uwekezaji katika Maonesho ya Wakulima ‘Nane Nane’ yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Benki ya Maendeleo ya TIB na baadhi ya wateja wake wanashiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa umma, kutangaza huduma inayozitoa pamoja na kuvutia wawekezaji kwa ajili ya uwekezaji wa kimkakati katika miradi mbalimbali hapa nchini.
Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Bima wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. James Manyama (kushoto) akitoa elimu ya Bima ya Kilimo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la TIB katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.
 Afisa Mwandamizi wa Usimamizi wa Miradi  wa Benki ya Maendeleo TIB, Bibi Mwajuma Milanzi (kushoto) akitoa maelezo ya Dirisha la Kilimo linalojihusisha na mikopo katika sekta ya kilimo  kwa mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la TIB katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya AMIMZA, Bw. Mustafa Mohammed akitoa maelezo ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo. Kampuni ya AMIMZA ni moja ya wateja wa Benki ya Maendeleo TIB waliopata fursa ya kutangaza bidhaa zao wakati wa   Maonesho ya Wakulima ‘Nane Nane’ yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.
 Afisa Masoko wa Kampuni Matongo Farming Co. Limited, Bw. Clement Lissawa (kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi aliotembelea Banda la TIB.
Mtaalamu wa Masuala wa Ufundi wa Kampuni ya Mwasonge, Bw. John Masero (kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi aliotembelea Banda la TIB.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad