HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 16, 2020

JKT Yatangaza Majina ya Vijana Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo Mwaka 2020


Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza majina ya vijana waliohitimu kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bara  waliochagulwa  kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2020 .
Akizungumza leo Julai 16, 2020 Makao Makuu ya Jeshi  hilo Wilayani Chamwino  Mkoani  Dodoma,  Mkuu wa Tawi la Utawala, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Julius  Kadawi amesema kuwa Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles  Mbuge anawakaribisha    waliochaguliwa  kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha , utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa kupitia mafunzo hayo.
“Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa, maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz”, Alisisitiza Kanali Kadawi
Aidha, Kanali Kadawi amesema kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 24 hadi 27 Julai, 2020 ambapo mafunzo yatafunguliwa rasmi Agosti 1, 2020.
Akifafanua, Kanali Kadawi amesema kuwa kwa upande wa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa  macho  (Physical disabilities) wanatakiwa kuripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa  jamii hiyo.
“Kutokana na Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID -19) nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama ilivyoelekezwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya zitazingatiwa kwa kipindi chote vijana watakapokuwa katika mafunzo”, Alisisitiza Kanali Kadawi
Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi  za JKT Rwamkoma- Mara, JKT Msange- Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa Dodoma, JKT Mafinga- Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba- Tanga, JKT  Makuyuni- Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, JKT Mtabila- Kigoma, JKT Itaka- Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa- Rukwa, JKT Nachingwea- Lindi,JKT Kibiti na Oljoro- Arusha.

Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Julius Kadawi  akitoa taarifa kuhusu kujiunga na mafunzo ya JKT mujibu wa sheria mwaka 2020 kwa vijana waliohitimu kidato cha sita katika shule za Tanzania Bara,  Taarifa hiyo ameitoa leo Makao Makuu ya Jeshi hilo  Wilayani Chamwino  Mkoani  Dodoma  Julai 16, 2020.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad