
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Simon Sirro, akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini miaka ya 1975 – 1980 Philemon Mgaya,
wakati wa serikali ya awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere.
Marehemu Philemon Mgaya alifariki dunia 14/07/2020 katika hospitali ya
Hindu Mandal jijini Dar es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika
tarehe 20/07/2020 Usangi, Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Simon Sirro (kusho) akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu
Omari Mahita, wakati walipoenda kutoa pole nyumbani kwa familia ya
aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini miaka ya 1975 – 1980 Philemon
Mgaya, Bahari Beach jijini Dar es salaam. Marehemu Philemon Mgaya
alifariki dunia 14/07/2020 katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar
es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 20/07/2020 Usangi,
Mwanga mkoani Kilimanjaro. Picha na Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment