Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akipongeza Kikundi cha
Utamaduni cha Nyati Mchoya (hawapo pichani) kwa namna wanavyorithisha
utamaduni kwa watato na vijana leo katika ziara ya kutoa elimu ya
uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa utamaduni katika Kijiji cha
Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma.
Kikundi cha Ngoma cha Nyati Mchoya kilichopo katika Kijiji cha
Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma kikicheza ngoma ya asili ya jamii ya
Wagogo mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
(hayupo pichani) leo katika ziara ya kutoa elimu ya uhifadhi na
uendelezaji wa urithi wa utamaduni.
Kikundi cha ngoma cha watoto cha kiitwacho Nyati C kikitoa burudani ya
ngoma mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutoa elimu ya uhifadhi na
uendelezaji wa urithi wa utamaduni iliyofanyika katika Kijiji cha
Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwa katika picha ya
pamoja na Kikundi cha Msamaria kutoka Kijiji cha Nzali mara baada ya
ziara ya kutoa elimu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Utamaduni
iliyofanyika leo katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma.
Kiongozi
wa Kikundi cha Nyati Mchoya Bw. John Mchoya akitoa ombi kwa Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hayupo pichani) la kusaidia baadhi
ya vikundi visivyo na uwezo wa kujisajili BASATA pamoja na kusaidia
vikundi vidogo kupata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali za
serikali na matamasha katika ziara ya kutoa Elimu ya Uhifadhi na
Uendelezaji wa Urithi wa Utamaduni iliyofanyika katika Kijiji cha
Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma.




********************************
Na Anitha Jonas – WHUSM, Chamwino
18/07/2020
Dodoma.
Wazee wa jamii za kitanzania
wasisitizwa kurithisha mambo ya utamaduni kwa watoto na vijana ili
tamaduni hizo ziweze kuendelea kwa vizazi vijavyo.
Wito huo umetolewa leo na
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu alipokuwa katika ziara
kutoa Elimu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Utamaduni
alipotembelea kikundi cha Utamaduni cha Nyati Mchoya, kilichopo katika
Kijiji cha Nzali, Kata ya Chilonwa, Dodoma.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri
mnayofanya ya kuwarithisha watoto na vijana shughuli za utamaduni hii
inasaidia mambo haya kuendelea hata kwa vizazi vijavyo na msipofanya
hivi mnahatarisha asili ya utamaduni wenu kupotea,”alisema Dkt.Temu.
Akiendeleza kuzungumza katika
ziara hiyo Dkt. Temu alisema kuwa serikali inataka kupanua wigo wa
utalii na kuifanya sekta ya Utamaduni kuwa ya utalii hivyo nijukumu la
kila mtanzania kulinda na kuhifadhi utamaduni wake kwani nchi hii
inautajiri mkubwa katika sekta hiyo ambao unaweza kukuza uchumi wa
mwananchi kwa urahisi zaidi kutoka na namna ya uendeshaji wake.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo
aliendelea kutoa wito kwa watanzania kuwa wanajitokeza kwenda kuangalia
burudani za utamaduni kama wanavyojitokeza kwenda kutazama mpira, na
kusema serikali inatarajia kuanzisha matamasha mbalimbali ya utamaduni
kwa lengo la kukuza na kutangaza utamaduni wa mtanzania.
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi
Maadili na Urithi wa Taifa Bw.Boniface Kadili alipongeza uongozi wa
vikundi vilivyotoa burudani ya ngoma kwa namna walivyonesha sanaa yao
kwa kuzingatia kuzingatia uchezaji wa asili ambao hauna kuiga watu wa
nje, zana za jadi walizotumia pamoja na uvaaji wa maleba.
Aidha, naye Kiongozi wa Kikundi
cha Nyati Mchoya Bw. John Mchoya alitoa ombi kwa wizara la kusaidia
baadhi ya vikundi visivyo na uwezo wa kujisajili BASATA pamoja na
kusaidia vikundi hivyo vidogo kupata fursa za kushiriki shughuli
mbalimbali ikiwemo matamasha na shughuli za serikali.
Halikadhalika nae mmoja wa kikundi
cha Msamaria Bibi. Rhoda Petro alishukuru uongozi wa wizara kwa
kuwatembelea na kuwa kutoa elimu ya namna ya kuhifadhi utamaduni wao na
kuwaomba kurudi tena wakati mwingine.
No comments:
Post a Comment