Wafanyakazi sasa kujiachia na riba hadi asilimia 14 kutoka Benki ya CRDB - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 1, 2020

Wafanyakazi sasa kujiachia na riba hadi asilimia 14 kutoka Benki ya CRDB

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiachie Utakavyo" ambapo wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi wataanza kufurahia riba ya hadi asilimia 14 huku wakiwa na uhuru wakuchagua muda wa kurejesha mkopo. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili (Wakwanza kushoto) na Meneja Mwanadamizi Mikopo ya Wafanyakazi, Farida Hamza.

=====   =====   =====

Benki ya CRDB imezindua kampeni maalumu ijulikanayo kama “Jiachie Utakavyo” ambapo wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi sasa kufurahia riba ya hadi asilimia 14. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati, Boma Raballa alisema benki imefanya maboresho makubwa katika mikopo ya wafanyakazi ili kuwapa unafuu na kuwawezesha kufikia malengo yao waliyojiwekea.

“Jiachie Utakavyo inamaanisha kuwa wafanyakazi sasa wana wigo mpana
zaidi wa kukopa, kwa gharama nafuu, kwa muda mrefu na uhuru wa
kuchagua wanachotaka,” alisema Boma Raballa.

Raballa alisema pamoja na kumpa uhuru mteja wa kujiachia kwa kuutumia
mkopo atakavyo, Benki ya CRDB pia imempa uhuru mteja kuchagua muda
wa kulipa mkopo anaoendana na matakwa yake na kiwango cha riba
anachotaka kulipa.
“Kwenye jiachie utakavyo mteja ana uhuru wa kuchagua muda wa kulipa iwe ni mwaka 1, 2, 3, mpaka 7, na vivile mteja atakuwa anachagua riba
anayotaka kuanzia asilimia 14 mpaka 16,” alisema Boma Raballa huku
akibainisha kuwa kampeni hiyo ya “Jiachie Utakavyo” inawapa fursa
wafanyakazi kukopa hadi shilingi milioni 100.

Akizungumzia kuhusiana na maboresho hayo ya mikopo ya wafanyakazi,
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili alisema Benki ya CRDB
inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wafanyakazi wa taasisi za
umma mna sekta binafsi, hivyo basi maboresho hayo ni motisha kwa
wafanyakazi kusaidia kufikia malengo yao.

“Tunafahamu changamoto tulizopitia katika kipindi hiki, na wafanyakazi wetu wamekuwa mstari wa mbele kukatika kutuhudumia katika kila nyanja,
kampeni hii ya Jiachie Utakavyo ni sehemu ya shukrani kwa wafanyakazi
wote, lakini pia kuwasaidia kufikia malengo yao,” alisema Adili.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiachie Utakavyo" ambap wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi wataanza kufurahia riba ya hadi asilimia 14 huku wakiwa na uhuru wakuchagua muda wa kurejesha mkopo.

Kwa upande wake Meneja mwandamizi Mikopo ya Wafanyakazi, Farida
Hamza alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyakazi wote nchini
kuchangamkia fursa hiyo ya “Jiachie Utakavyo”, huku akibainisha kuwa mteja ana uhuru wa kutumia mikopo hiyo atakavyo ikiwa ni pamoja na kulipia ada za Watoto, kijiendeleza kimasomo, kuanzisha na kuendeleza biashara na matumizi mengine apendayo.

“Mikopo hii si kwa wateja wa Benki ya CRDB tu ni kwa wafanyakazi wote
nchini, kama mfanyakazi anamkopo benki nyengine, Benki ya CRDB
inautaratibu wa kununua mikopo ili kuwafanya wafanyakazi wote waweze
kujiachia watakavyo na Benki yao pendwa ya CRDB,” alisema Farida huku
akibainisha mikopo hiyo inatolewa ndani ya saa 24 mteja napokamilisha
maombi ya mkopo.

Ili kupata mkopo huo wafanyakazi wanatakiwa kutembelea tawi la Benki ya
CRDB lililo karibu na kujaza fomu ya maombi ya mkopo ambapo atatakiwa
kuambatanisha vielelezo vifuatavyo; Kitambulisho kinachotambuliwa - cha
utaifa/ kura/ leseni ya udereva na kitambulisho cha kazi, Hati ya mshahara
(Salary slip) iliyothibitishwa kwa kipindi cha miezi mitatu, Mkataba wa kazi/
barua ya uteuzi, barua ya utambulisho, barua ya uthibitisho kazini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad