HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 23, 2020

Fundi 24/7- Soko mtandaoni

Na Godwin Semunyu
Maendeleo ya mifumo ya habari na mawasiliano yameleta mabadiliko mengi chanya kwenye Maisha ya binadamu. Sifa kubwa ya mifumo hiyo ni upatikanaji wa bidhaa na huduma kwa uharaka na uthabiti zaidi.

Fundi 24/7 ni mtandao wa kitanzania unaowakutanisha wateja na mafundi watoa huduma mbalimbali nchini kwa njia ya  mtandao na hivyo kuokoa muda wa wote wawili. “Lengo kuu la kuanzisha huduma hii ya Fundi 24/7 ni kuwakutasha wateja na mafundi ili kutoa huduma kwa uharaka. Kupitia mfumo huu, mteja anaweza kumuita fundi wa ujenzi, magari, mabomba, umeme na wengineo bila kuhitaji kutoka nyumbani” anasema Martin Warioba Mkurugenzi wa mtandao huo.

Warioba anasema kuwa zaidi ya kuwakutanisha wateja na mafundi, mtandao huo pia unawajumuisha watoa huduma kama wenye maduka ya vifaa vya ujenzi au vipuri vya magari. “Mtu anaweza kupata fundi kupitia mtandao wetu, akanunua kifaa husika kupitia mtandao wetu na kisha kulipa kidijitali kwa kutumia mtandao wa simu. Haya yote yanaweza kufanyika kwa kutumia fundi 24/7 huku ukiwa nyumbani” alisema.
Warioba anaendelea kusema kuwa mfumo wa Fundi 24/7 hutumia Global Position System (GPS) hivyo kumsaidia mteja kupata fundi aliye karibu zaidi wakati wa uhitaji: “Kwa kutumia GPS, wateja wenye Fundi 24/7 wana uwezo wa kupata mafundi hapo hapo walipo.

Mathalan, kama uko safarini na ukaharibikiwa gari eneo la Msata, mfumo wetu utawapa taarifa mafundi wote wa magari waliopo karibu na eneo husika, na wewe utachagua yupi aje kukuhumidumia kwa uharaka. Pia Malipo yote ya huduma yatafanyika kidijitali hivyo mteja hatahitaji pesa taslimu” alisema.

Warioba anasema kuwa huduma za Fundi 24/7 zinaweza kupatikana kwa kupakua application yake kupitia Google Play Store na Apple Store kupitia simu za mkononi au Kompyuta zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad