ULEGA AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI 140 NA MIL.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 13, 2020

ULEGA AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI 140 NA MIL.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO


 Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga ambae pia ni Naibu wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega amekabidhi sh.milioni tatu na mifuko ya saruji 140 kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo Jimbo la Mkuranga. 

Zoezi hilo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi mbalimbali alizozitoa mbunge Ulega kwenye miradi ya maendeleo.

Miradi iliyonufaika ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Lukanga saruji mifuko 50, ujenzi wa zahanati Yavayava saruji mifuko 50, ujenzi wa kivuko Churwi 30, ujenzi wa zahanati Kisiju mifuko kumi, ujenzi wa ofisi ya kijiji Kiziko sh.500,000,ujenzi wa Ofisi kitongoji cha Mkoga 500,000, na ujenzi wa ofisi Tungi sh.200,000. 


Miradi ya ujenzi wa ofisi za Chama cha Mapinduzi iliyonufaika na utekelezaji huo ni ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kisiju 400,000, ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Mfulu Mwambao 400,000 na ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Vianzi 400,000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad