HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 21, 2020

RPC TANGA AWAONYA WEZI,AWAAMBIA WATAKAOKAMATWA WATAFINYANGWA FINYANGWA WASAHAU WALIPOTOKEA


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali.
 Camera ambazo pia zimekatwa wakati wa operesheni hiyo.
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP), Blasius Chatanda akiwaonyesha waandishi wa habari vitu ambavyo
vimekamatwa wakati wa opeseheni hiyo.
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda ametoa onyo kali kwa wezi wanaovunja nyumba za watu na kuiba mali kwa kuwataka waache mara moja tabia hiyo kabla
hawajafinyangwa finyangwa.

Chatanda aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba awali kulikuwa kumeibuka wimbi la uvunjaji wa nyumba hali ambayo iliwalazimu kuanzisha operesheni kabambe ya kuwasaka ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.

Alisema kwamba katika operesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 8 ambao kwa sasa wapo mahabusu ambapo walikamatwa wakiwa na vitu mbalimbali ambavyo waliviiba kwenye maeneo mbalimbali  Jijini Tanga.

Kamanda Chatanda alitaja vitu ambavyo vilikamatwa kuwa ni TV Flat Screen 7zenye ukubwa wa tofauti kuanzia nch 50 hadi 21 ambazo zinadaiwa ziliibiwa kwenye baadhi nyumba za kulala wageni zilizopo Jijini Tanga.

Aidha alisema pia katika operesheni hiyo waliwakamata vitu vingine ikiwemo Kompyuta mpakato  16,simu za mkononi 7 ambapo baadhi ya vitu hivyo viliibiwa kwenye nyumba
za kulala wageni.

“Tunaomba walioibiwa waje watambue mali zao kama ni miongoni mwa zilizokamatwa huku akisisitiza kwamba msako huo ni endelevu na hakuna mtu ambaye hatabaki salama “Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.

Kamanda huyo alisema kwamba msako huo ni endelevu na
hakuna mtu ambaye atabaki salama huku akieleza kwamba kwa waliozoea
kuiba watafute kazi nyengine za kufanya kwa sababu wakikamatwa
watawafinyangwafinyanwga mpaka wasahau njia walizokujia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad