MKAZI WA MASAKI, MNAIGERIA KIZIMBANI KWA KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 24, 2020

MKAZI WA MASAKI, MNAIGERIA KIZIMBANI KWA KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

 Washtakiwa, David Chukwu raia wa Nigeria, Isso Lupembe, wa Mbezi Luis na Allistair Mbele  wakiwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza kusomewa kesi inayowakabili  ya kusafirisha dawa za kulevya na kutakatisha fedha zaidi ya Sh. Milioni 50 ambapo wate wamerudishwa rumande kwa kuwa kesi inayowakabili haina dhamana.
 Washtakiwa, David Chukwu raia wa Nigeria, Isso Lupembe, wa Mbezi Luis na Allistair Mbele wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

WAFANYABIASHARA watatu akiwemo Raia mmoja wa Nigeria, David Chukwu 38 Mkazi wa Masaki wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilogramu 268.50 za dawa za kulevya na kutakatisha zaidi ya sh. Milioni 150.


Mbali na Chukwu washtakiwa wengine ni Isso Lupembe 49 mkazi wa Mbezi Luis na Allistair Mbele 38 anayeishi Mbezi Kibanda cha Mkaa.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali waandamizi , Veronika Matikila, na Wankyo Simon pamoja na wakili wa serikali Batlida Mushi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Geoffrey Issaya washtakiwa katika kosa la kwanza wanashtakiwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili Batlida amedai kuwa, Aprili 4, mwaka 2020 huko katika eneo la Mbezi Kibanda cha Mkaa ndani ya Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilogramu 268.50 .

Aidha katika shtaka la pili lililosomwa na wakili mwandamizi Wankyo imedaiwa kuwa, kati ya Januari 2016 na Aprili 15 2020 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, washtakiwa hao walijihusisha katika miamala iliyohusisha fedha  USD 61,500 na fedha za kitanzania Sh. 17,835, 500  huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kusafirishi dawa za kulevya.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo na wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 8 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Aidha upande wa mashtaka umesema kutoka na uwepo wa ugonjwa hatari wa homa ya mapafu (CORONA)  wameishawapima washtakiwa wote watatu na wako salama na hivyo wanaweza kwenda

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad