HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 24, 2020

ABIRIA WASIOVAA BARAKOA WAONYWA, NDIKILO APOKEA MSAADA WA MATENKI 25


 Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepokea vifaa vya Kunawia Mikono ,tenki 25 za maji kutoka Kampuni ya Motisun Group vyenye thamani ya Sh.6.2 ikiwa ni jitihada za Mkoa kushirikiana na Wadau katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Ndikilo ametumia pia,wasaa huo kuwakumbusha na kuwaonya baadhi ya abiria wanaokaidi agizo la kuvaa barakoa ambalo wataalamu wa afya wamekuwa wakielekeza ili kupunguza maaambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.

Akizungumza wakati wa upokeaji wa vifaa hivyo ,alisema vifaa hivyo vitagawanywa katika Hospitali  ya Mkoa na za Wilaya,  Kituo cha Matibabu ya Covid 19 Lulanzi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri ,Masoko,Kituo Cha Afya Mkoani, Mlandizi ,Kibiti, pamoja  na Shirika la Nyumbu  .

" Wananchi tuvae barakoa na kuzingatia level sit kwenye vyombo vya safari hii ni kwa afya zetu hata mkisimama  si kwa hasara ya mtu mwingine ni wewe na familia yako" alisema Ndikilo.

Ndikilo alielekeza wahusika katika Mkoa huo kufuatilia suala hilo kwani kwa kuendelea kuwaacha baadhi ya watu wakisafiri bila kuvaa barakoa ni Moja ya Maeneo ambayo yana uwezekano wa kuambukizana.

Aidha, alisema kwa sasa wazazi watunze watoto wao wasizurure mtaani kwa hali ilivyo ambayo ni hatari.

Hata hivyo, Ndikilo aliwakumbusha wazazi  kuwa Serikali imefunga Shule hivyo amewataka kuzuia watoto wao kuzurura Mitaani.

Nae ofisa Uhusiano wa Kampuni ya M.M.I Steel Abubakar Mlawa ,alisema msaada huo wa tanki unaenda sambamba na misaada mengine ya matanki 1,000 ambayo wameshaitoa katika maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad