Ubongo yatoa programu za watoto kujifunza majumbani wakati shule zimefungwa kutokana na ugonjwa wa corona - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 24, 2020

Ubongo yatoa programu za watoto kujifunza majumbani wakati shule zimefungwa kutokana na ugonjwa wa corona

Katika kuunga mkono juhudi za kupambana na usambaaji wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona, taasisi ya Ubongo, ambayo inayoongoza barani Afrika kwa kutengeneza vipindi kwa njia ya kidigitali kwa ajili ya kufundisha watoto wa rika mbalimbali kwa njia ya mfumo wa elimu-burudani imesema kuwa itatoa ushirikiano mkubwa katika kuchukua hatua madhubuti na kuwaunga mkono walezi na watoto kuendelea kujifunza nyumbani wakati shule zimefungwa.

Takwimu zilizotolewa na shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema idadi ya watoto waliopo mashuleni ambao wamepata maambukizi ya virusi vya korona yameongezeka hadi kufikia 849 hadi Machi 18, kutoka wagonjwa 102.

Kwa kutumia mfumo wa kisasa kabisa wa kidigitali, taasisi ya Ubongo inatoa bure maktaba ya maudhui kwa Watoto na walezi ambayo inagusua mada nyingi kwa upana zaidi, ambayo itaweza kutazamwa na kupatikana katika lugha nyingi za kiafrika.

Wazazi, walimu, walezi na watoto wamehimizwa kutumia mfumo huu wa kimtandao pamoja na runinga na redio ambapo mtiririko wa mada za Ubongo utakuwa unarushwa hewani.

Kwa upande wa Tanzania, vipindi vya Akili na mimi vinavyorushwa na kituo cha runinga cha TBC1 siku ya jumamosi na jumapili saa tatu asubuhi, kwenye kituo cha runinga cha EATV hurushwa kila siku ya jumamosi saa 6:30.

Vipindi vya watoto vya Ubongo hurushwa baada ya Akili na mimi kuanzia saa tatu na nusu asubuhi katika kituo cha runinga cha TBC1 siku za Mwisho wa wiki na siku ya alhamisi saa 4:30 kwa upande wa kituo cha runinga cha EATC.

“Tunafanya kazi kwa bidii sana kaka wadau katika sekta ya elimu ili kuweza kukabiliana na tatizo la korona kwa njia bora zaidi kwa kutoa maudhui ambayo itatoa elimu juu ya njia salama zaidi ya kukabiliana na tatizo hili.

Baada ya kuzindua jukwaa la Ubongo mwanzoni mwa mwezi huu sasa juhudi kubwa imewekwa katika kuutangaza hasa kwa Wazazi ili wautumie kwa Watoto wakiwa nyumbani.

Tunatoa bure maktaba yetu ya runinga na redio kwa watangaji wote na wadau ambao wanaweza kushirikiana na jamiii pamoja na huduma za matangazo na video za elimu ili kuchangia sekta ya afya na usafi.

Hatua hizi zote zinafanywa na taasisi ya Ubongo ili kutoa elimu kwa Watoto wote,” alisema Afisa Bidhaa Mkuu wa taasisi ya Ubongo, Christina Bwana.

Ubongo ina maktaba kubwa yenye ubora na ambayo imetenezwa afrika, ina maudhui ya hali ya juu kwa ajili ya Watoto wenye umri kuanzia Mwaka 0 hadi 14 na walezi.

Maktaba hii inagusa mada nyingi kuanzia hatua ya awali ya kujifunza kuhesabu, kujifunza kusoma pamoja na ujuzi hadi ule wa kihandisi, sayansi na tekinolojia.

Nyenzo hizi za kujifunzia zipo katika lugha zote mbili za Kiswahili na kiingereza na pia toleo limefanyika katika lugha ya Kinyarwanda, Hausa, Luo na Chichewa.

Vifaa hivi vya kujifunzia hutumika kama nyenzo ya kufundishia ili kuweza kuboresha namna ya ufundishaji kwa kutumia njia ya video na sauti.

“Tunafanyia kazi namna ya kuunganisha maudhui na rasilimali za kujifunzia pamoja na vitabu mtandao, programme nyingine na mitaala kutoka shule za awali hadi gredi ya 7 katika nchi za afrika ambapo shule zimefungwa.

Tumeelekeza Nguvu zaidi katika nchi za Tanzania, Rwanda na Kenya kama soko letu kubwa. Hii itasaidia familia kupata maudhui sahihi kwa ajili ya Watoto wao kwa ajili ya kujifunza majumbani,”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad