NBC YAUNGA MKONO SEKTA YA KILIMO MKOANI LINDI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 10, 2020

NBC YAUNGA MKONO SEKTA YA KILIMO MKOANI LINDI

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) yazindua NBC B Club Katika mkoa wa Lindkwa lengo la kuunga mkono sekta ya kilimo ambapo kuna zao la Korosho na Ufuta na msimu wake unakaribia kuanza. 

Mazao hayo mawili ni kati ya mazao makubwa ya kibiashara yanayofanyika katika nchi yetu na nje ya nchi ya Tanzania. 

Kongamano hilo lilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja mbali na kwa pamoja walipata kufahamu fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wanachama wa Biashara Club. 

Akizungumza na wafanyabiashara, Meneja wa bidhaa na huduma za kifedha NBC Makao makuu Dar es salaam, Jonathan Bitababaje amesema, kuwa benki hiyo imedhamiria kurahisisha huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali hususani wafanyabiashara ambao ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini.

Amesema vilabu vya Biashara vya NBC hutumiwa kama sehemu ya utunzaji wa biashara na mkakati wa uaminifu wa wateja. Kusudi kuu ni kuwakutanisha wafanya biashara na kuwaunga mkono  kwenye fursa mbali mbali zilipo katika mkoa huo.. 

"NBC B Club ni mahali muafaka pa kuelimisha wafanyabiashara juu ya masuala mbalimbali kuhusu biashara na tangu kuanzishwa kwa klabu hizi za biashara, wanachama wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kutumia vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini TRA," amesema na kuongeza.

Jonathan Bitababaje, amesema lengo kuu kwa mkoa wa Lindi ni kuunga mkono sekta ya kilimo ambapo kuna zao la Korosho na Ufuta na msimu wake unakaribia kuanza. Mazao hayo mawili ni kati ya mazao makubwa ya kibiashara yanayofanyika katika nchi yetu na nje ya nchi ya Tanzania. 

‘’Mfanyabiashara akiwa mwanachama wa klabu hizo atapata Mikopo ya Muda, Huduma za ziada, Ufundi wa kigeni, POS, Benki ya mtandao, Akaunti za sasa, Dhamana za Benki, Benki ya Wakala, na Bidhaa za Bima.’’ amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga ambaye alikua mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa klabu hiyo alipongeza NBC kwa kuamua kuwaunga mkono wafanyabiashara katika kukuza sekta ya kilimo.

‘’ Sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha yoyote ambaye ana nia ya kuwekeza hapati changamoto yoyote itayomfanya ashindwe kuwekeza. Njooni tuambieni mnataka ardhi kufanya kitu fulani na naomba niwahikikishie kwa manufaa ya Lindi tunayo timu nzuri sana ambayo inashughulikia swala zima la uwekezaji.’’ alisema.

Shaibu Ndemanga amesema lengo lao ni kuhakikisha uwekezaji huo ubebwe wa watu wa Lindi kwanza. ‘’ Hakuna dhambi wewe kuanzisha, anaekuja akaingia ubia na wewe” Aliendelea kusema kuna fursa ambazo zinakuja na angependa watu wa Lindi waone jinsi watavyo tumia izi fursa kuptia NBC.

Aidha amemalizia kwa kukusema anataka kuona wana Lindi wamejipange kuchangamkia fursa hizi na aliishukuru NBC kwa kuona fursa katika mkoa huo na kwa kujitoa kwao kusaidia wana Lindi wa kuunga mkoo sekta ya kilimo.

Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, NBC Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.

Aidha benki hiyo imeendesha mafunzo ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kubwa kwa lengo la kuwaongezea uwezo, uelewa na ubunifu katika ufanyaji wa biashara zao.
Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha wa NBC, Nd. Jonathan Wilson akizungumza na wafanya biashara wa Mkoa wa Lindi wakati wa uzinduzi wa NBC Business Club kwa Mkoa wa Lindi. NBC Business Club kwa sasa imeenea katika mikoa mbali mbali nchini ikiwemo Singida, Morogoro, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Njombe,M Mbeyapamoja na Tanga ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha, kuwaongezea ujuzi na kuwakuzia  mtandao wafanyabiashara.
  Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga (Kushoto), akisalimiana kwa kugonganisha miguu na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Lindi, Nd. Hamisi Livembe wakati wa uzinduzi wa NBC Business Club kwa Mkoa wa Lindi.NBC Business Club kwa sasa imeenea katika mikoa mbali mbali nchini ikiwemo Singida, Morogoro, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Njombe, Mbeya pamoja na Tanga ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha, kuwaongezea ujuzi na kuwakuzia  mtandao wafanyabiashara. Wengine katika picha ni Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha NBC, Nd. Jonathan Wilson (wa pili kushoto) na Meneja wa Tawi NBC Lindi Ndg. Iovin Mapunda (Kulia).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad