WAKANDARASI NA WAZABUNI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA FEDHA NDANI YA BENKI YA CRDB - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 13 December 2019

WAKANDARASI NA WAZABUNI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA FEDHA NDANI YA BENKI YA CRDB

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga. Kongamano hilo liliratibiwa na Benki ya CRDB. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, Mkuu wa Mkoa Geita, Injinia Robert Gabriel, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, Meneja wa Kanda ya Magharibi Benki ya CRDB, Saidi Pamui, Meneja wa Kanda ya Ziwa Benki ya CRDB, Lusing Sitta

Na Mwandishi wetu.

Benki ya CRDB imeandaa kongamano maalum la uwezeshaji kibiashara kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wa ujenzi wa miradi ya maendeleo kanda ya Magharibi ikihusisha mikoa ya Shinyanga, Geita, Tabora na Kigoma.

Kongamano hilo ambalo limekutanisha wadau mbalimbali wa miradi ya maendeleo ikiwemo makampuni zaidi ya 350 pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali ikiwamo, lilifunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo wakuu wa mikoa wa kanda hiyo.

Akitoa hotuba yake wakati wa kufungua kongamano hilo, Bashungwa, amewataka wakandarasi kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuacha kutegemea malipo ya awali ya mradi husika ambazo zimekuwa zikichelewa na kufanya miradi kutokamilika kwa wakati.

“Benki ya CRDB imewaletea fursa mlangoni, itumieni vilivyo, changamkieni fursa hizo ili muweze kukuza biashara zenu na kupata faida zaidi, kuongeza ajira kwa vijana wetu na hatimaye kulipa kodi stahiki za serikali.” alisema  Bashungwa.

Bashungwa pia alipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa miondombinu mbalimbali ambayo itasadia kuchochea ukuaji wa uchumi. “Tunatambua na kuthamini sana ushikiri wa Benki ya CRDB katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini, hongereni sana,” aliongeza Waziri Bashungwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ya Kanda ziwa, Aggrey Mwanri aliwahamasisha wakandarasi na wazabuni wa miradi ya maendeleo katika mikoa ya kanda hiyo ya magharibi kuchangamia fursa zinazotolewa na Benki yetu ya CRDB, ili kwa kushirikiana na serikali waweze lengo la kuimarisha miundombinu nchini.

Akizungumza katika kongamano hilo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alimhakikishia Mheshimiwa Bashungwa kuwa Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” imejipanga vilivyo katika kuhakikisha inashirikiana na Serikali kutimiza azma ya ujenzi wa uchumi wa kati unoshamirishwa na viwanda kupitia uwezeshaji wa miradi mbalimbali nchini.

Dkt. Witts alisema Benki ya CRDB imejipanga vilivyo kuwahudumia Wakandarasi nchini huku akitaja baadhi ya huduma ikawamo huduma ya dhamana kwa wakandarasi au wazabuni ambao wanatafuta kazi ijulikanayo kama “Bid Guarantee” dhamana za utekelezaji wa miradi “Performance Guarantee” na dhamana za malipo ya awali “Advance Payment Guarantee”.

Dkt. Witts alisema Benki ya CRDB pia imeboresha taratibu zake za utoaji mikopo na hivyo kuwasihi Wakandarasi hao kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo, kufungua akaunti, pamoja na kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na majanga yanayoweza kutokea. “Benki ya CRDB ni Benki yenu, na sisi tupo hapa kuwahudumia niwahakikishie tu sisi Tupo Tayari kuwahudumia,” alihitimisha Dkt. Witts.

Akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ukandarasi ya Junior Construction Ltd na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi aliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo ya kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi nchini huku wakieleza fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB zitakwenda kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akihutubia wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akihutubia wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wajasiriamali kwa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi akichangia wakati wa kongamano hilo la wakandarasi na wazabuni wa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora lililofanyika Desemba 12, 2019, mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad