WATANZANIA KUNUFAIKA NA VIFURUSHI VYA BIMA YA AFYA ITAKAYOZINDULIWA KESHO, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 27 November 2019

WATANZANIA KUNUFAIKA NA VIFURUSHI VYA BIMA YA AFYA ITAKAYOZINDULIWA KESHO, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Novemba 28, 2019 unatarajia kuzindua rasmi vifurushi vya bima ya afya ili kuwapa fursa wananchi wengi kujiunga na kunufaika na huduma za bima hiyo kulingana na mahitaji yao na kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote.Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya vifurushiaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga amesema, vifurushi hivyo vinatoa fursa kwa mtu mmoja mmoja, familia au makundi mbali mbali ya wananchi kujiunga na huduma hizo.

"Mpango huu wa vifurushi utawezesha wananchi wengi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha na hivyo kukabiliana na gharama za matibabu ambazo garama yake imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na ambazo wakati mwingine kushindwa kuzimudu kwa wakati", amesema Konga.

Amesema, mpango huo wa Vifurushi vya bima ya afya unatoa uwanja mpana wa wananchi kujiunga na bima ya afya kwa kujipimia kulingana na mahitaji ya huduma, ukubwa wa familia na umri. Vifurushi hivi vimegawanywa katika makundi matatu yanayojulikana kama Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya.

"Kuanza kwa mpango huu kumekuja baada ya kuona uhitaji uliopa katika umma wa kuwa na uwigo mpana wa wananchi kujiunga na Mfuko huu. Hitaji la huduma hizi limedhihirika wazi baada ya kufanya majaribio ya mpango huu(Pilot test) mwezi Septemba mwaka huu kwa muda wa wiki tatu ambapo mwitikio ulikuwa mkubwa kutoka kwa wananchi. Tathmini ya majaribio hayo ilitoa nafasi ya kufanya maboresho mbalimbali ya mpango huu na sasa uko tayari kwa ajili ya kuletwa kwa wananchi," amesema 

Amesema viwango vya uchangiaji wa vifurushi hivi vinaanzia 192,000 kumezingatia hali halisi ya makundi yote na kutawezesha Watanzania wengi zaidi kujiunga na Mfuko na kuwa na uhakika wa kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapougua hivyo kuondokana na changamoto za kukosa matibabu.

Aidha, uanzishwaji wa mpango wa vifurushi unawawezesha wananchi wengi zaidi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha. 

Hivyo, kutokana na maboresho haya, amesema wananchi wana fursa ya kukabiliana na gharama za matibabu ambazo zimekua zikiongezeka siku hadi siku na wakati mwingine kushindwa kuzimudu na kuangukia katika janga la umaskini au kifo.

"Kuanza kwa mpango huu ambao viwango vyake vya uchangiaji vinaanzia 192,000 kumezingatia hali halisi ya makundi yote na kutawezesha Watanzania wengi zaidi kujiunga na kuwa na uhakika wa kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapougua hivyo kuondokana na changamoto za kukosa matibabu," amesema

Aidha, uanzishwaji wa mpango wa vifurushi unawawezesha wananchi wengi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha. Hivyo, kutokana na maboresho haya, wananchi wana fursa ya kukabiliana na gharama za matibabu ambazo zimekua zikiongezeka siku hadi siku na wakati mwingine kushindwa kuzimudu na kuangukia katika janga la umaskini au kifo.

Amesema, vifurushi hivi vitasaidia wananchi wenye kujali afya zao na kuwa na uhakika wa kupata huduma mwaka mzima ambapo mwanachama atapatiwa kadi ya matibabu ya Mfuko ambayo ataitumia kupata huduma katika vituo zaidi ya 7,500 vilivyosajiliwa na mfuko nchini.

"Wanachama wa vifurushi hivi watanufaika na huduma za matibabu kuanzia ngazi ya zahanati hadi Hospitali ya Rufaa ya Taifa katika vituo zaidi ya 7,500 Tanzania nzima ikiwa ni vya Serikali, Binafsi na vya Madhehebu ya Dini. Aidha, mwanachama atakwenda ngazi ya Hospitali ya Kanda ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Taifa kwa utaratibu wa rufaa," amesema.

Amesema vifurushi vyote vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya vimezingatia upana wa huduma kwa mwananchi ikiwa ni kuanzia gharama za kumwona daktari, vipimo, dawa, kulanza, upasuaji mkubwa na mdogo, matibabu ya kinywa na meno na mengineyo. Ukubwa wa kitita cha mafao utazingatia aina ya kufurushi ambacho mtu atachagua..
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Bw. Bernard Konga akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika hilo zilizopo jengo la Ushirika jijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza uzinduzi wa vifurushi vipya vya bima ya afya vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya vitakavyozinduliwa kesho kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Kulia ni Baraka Maduhu Meneja Takwimu na Utafiti (NHIF) na katikati ni Bi. Angella Mziray Meneja uhusiano wa (NHIF)
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Bw. Bernald Konga wa pili kutoka kushoto akimzikiliza Bi. Angella Mziray Meneja uhusiano wa (NHIF) wakati alipokuwa akitambulisha wakuu wa vitengo mbalimbali wawa NHIF walioshiriki katika mkutano katika ya shirika hilo na waandishi wa habari leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Bw. Bernard Konga akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vitengo mbaimbali wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mara baada ya mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad