TAASISI YA DORIS MOLLEL YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 18 November 2019

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea maelezo kutoka kwa Muuguzi kiongozi katika Wadi ya Watoto Njiti, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Cleopatra Mtei (kushoto), wakati alipotembelea Wadi hiyo baada ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti yaliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel, Novemba 14, 2019. Wengine ni Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe (wa pili kulia), Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (katikati) na kulia ni Dkt. Isaack Maro.
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini, akimkabidhi zawadi mmoja wa Mama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti), Felista Nyambala, wakati alipotembelea Wadi hiyo Novemba 15, 2019, Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es salaam. Katikati ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel pamoja na Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe.
Mama Getrude Mongela ambaye ni Mwanadiplomasia nguli na mpiganaji wa haki za wanawake aliyekua Mgeni wa heshima katika kafla hiyo fupi  akizungumza, Mama Mongela alifika hapo ili kuona na kujadili changamoto zinazowakumba wazazi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), likiwemo swala la likizo ya uzazi, alisema anatambua changamoto za Watoto Njiti kwani Mmoja wa Wajukuu zake alizaliwa akiwa Njiti. Katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini na kushoto ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel.
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Novemba 14, 2019, Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad