SERIKALI KUTOA MILIONI 300 KWA AJILI YA MRADI WA KUSAMBAZIA MAJI WANANCHI KUTOKA BWAWA LA TURA WILAYANI UYUI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 4 November 2019

SERIKALI KUTOA MILIONI 300 KWA AJILI YA MRADI WA KUSAMBAZIA MAJI WANANCHI KUTOKA BWAWA LA TURA WILAYANI UYUI

Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongozana jana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Uyui kutoka Bwawa la Tura wilayani Uyui ambapo ametoa milioni 300 kwa ajili ya kuanza ujenzi mradi wa usambazaji maji katika eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Igalula Mussa Ntimizi akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa(mwenye kofia) jana wakati kiongozi wakati alipokuwa na ziara ya kukagua Bwawa la Tura wilayani Uyui ili kuona jinsi ya kujenga mradi wa kusambaza maji.

SERIKALI imeahidi kutoa milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa usambazaji wa maji kwa wananchi kutoka chanzo cha maji cha Tura wilayani Uyui ili kuwaondolea kero ya upatikanaji wa maji ya uhakika ya muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo.

Fedha hizo ni sehemu zitakazotumika katika kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara yake Wilayani Uyui Mkoani Tabora kwa ajili ya kutatua kero za maji kwa wananchi wa eneo hilo.

Alisema kukamilika kwa chanzo hicho cha maji kitasaidia kuzalisha lita zaidi ya milioni 2.7 na kuwahudumia wakazi zaidi ya 11,000 na hivyo kuwaondolea usumbufu wa kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Alisema kuwa Serikali haiwezi kuona wananchi wanateseka kutafuta maji kwa umbali mrefu huku kukikwa na chanzo cha maji kizuri ambacho hakitumiki.

Waziri huyo alisema mradi huo utakuwa na hatua tatu ambazo ni ujenzi wa kituo cha kutoa maji kwenye bwawa na kusafisha maji, hatua ya pili ni ujenzi wa tenki la upokeaji wa maji na hatua ya mwisho ni ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji kwa wananchi.

Naye Mbunge wa Jimbo Igalula Mussa Ntimizi alisema kuwa licha ya bwawa hilo kumilikiwa na Shirika la Reli Tanzania(TRL) wamekubaliwa lianze kutumika kutatua kero ya maji kwa wananchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad