MBUNGE KINGU AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO , AWAHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 4 November 2019

MBUNGE KINGU AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO , AWAHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

Mbunge Kingu akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakati akikagua ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kijiji cha Nkenene.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akiwahubia wananchi wa Kijiji cha Ilowoko wakati akikagua miradi ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katibu Muenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Iyumbu, Lameck Maguni akizungumza kwenye mkutano huo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkenene wakiwa kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Kijiji cha Nkenene wakiwa kwenye mkutano.
Mbunge Kingu akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Ilowoko.
Mbunge Kingu akiwa na Wananchi baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kijiji cha Ilowoko. 

Na Dotto Mwaibale, Singida
WANANCHI wa Kijiji cha Ilowoko Kata ya Iyumbu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamesema hawajawahi kumuona mbunge anayewajali wananchi wanaoishi maporini kama Elibariki Kingu.

Hayo waliyasema juzi katika mkutano wa hadhara aliouandaa mbunge huyo wakati akikagua miradi ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

"Kwa kweli tangu kijiji hiki kianzishwe hatujawahi kumuona kiongozi yeyote anayejali wananchi wanaoishi maporini kama mbunge huyu Elibariki Kingu" alisema mkazi wa kijiji hicho aliyejitambilisha kwa jina moja la Nkuba 

Nkuba alisema viongozi waliowengi wanapenda kuwatembelea wananchi ambao wapo maeneo yanayofikika kiurahisi kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mizuri lakini kwa Kingu amefanikiwa katika hilo.

Kingu akizungumza katika mkutano huo alisema tangu Rais Dkt. John Magufuli aingie madarakani amefanya kazi kubwa ya kuwaletea watanzania maendeleo.Alisema amewapelekea miradi ya maji, ujenzi wa vituo vya afya Ihanja, Sepuka na sasa katoa sh.500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Iyumbu.

Kingu alisema kuwa mbali na miradi hiyo pia amefanikisha kujenga shule, barabara na baadhi ya maeneo yamepata umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)

Kingu alisema kutokana na kazi hiyo kubwa aliyoifanya Rais Dkt. John Magufuli kwa wananchi hao heshima ya pekee ya kumpa watahakikisha viongozi wote katika uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

" Ndugu wananchi heshima pekee ya kumshukuru Rais wetu kwa kutuletea maendeleo haya ni kuhakikisha tunakipa ushindi mkubwa chama chetu naombeni twendeni tukajiandikishe kwa wingi na siku ikifika ya kupiga kura basi tuwachague viongozi watakaounda serikali kupitia CCM" alisema Kingu.

Katika Kata hiyo ya Iyumbu Kingu alitoa zaidi ya sh.700,000 kwa ajili ya kukarabati madawati ya Shule ya Msingi Nkenene na ujenzi wa sakafu wa shule hiyo ambayo imechakaa hivyo kuwafanya wanafunzi kupata elimu kwenye mazingira duni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad