MIFUMO IMEKUWA CHANGAMOTO KWA MWANAMKE KUSHIRIKI TAFITI ZA KISAYANSI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 15 November 2019

MIFUMO IMEKUWA CHANGAMOTO KWA MWANAMKE KUSHIRIKI TAFITI ZA KISAYANSIMkurugenzi Mkuu Mtandao wa sayansi na teknolojia kwa nchi za Afrika, Dkt. Nicholas Ozor kulia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa wanawake katika Tafiti za Kisayansi na ubunifu katika mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya utafiti Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Profesa Mohamed Sheikhe.
 Afisa Mtafiti Mwandamizi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Hildegalda Mushi kushoto, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya utafiti Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Profesa Mohamed Sheikhe na watatu ni Mkurugenzi Mkuu Mtandao wa sayansi na teknolojia kwa nchi za Afrika, Dkt. Nicholas Ozor.
 Taasisi ya Sayansi ya Taifa-US, Makyaba Charles-Ayinde akizungumza na waandishi wa habari katika Makutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtandao wa sayansi na teknolojia kwa nchi za Afrika, Dkt. Nicholas Ozor.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya utafiti Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Profesa Mohamed Sheikhe akizungumza na waandishi wa habri jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na wanasayansi kutoka nchi15 za kusini mwa jangwa la Sahara na kutoka nchi mbalimbali. kushoto ni

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
MIFUMO ya utoaji fedha za kitafiti na mifumo ya elimu imekuwa changamoto kwa wanawake kushiriki katika tafiti za kisayasi, teknolojia na ubunifu kwasababu ya kutokuwepo na vigezo vinavyompa kipaumbele mwanamke.

Afisa Mtafiti Mwandamizi Hildegalda Mushi, ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea kufanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa kuanzia ngazi za chini za elimu wanamke anapojifunza  anakuwa na changamoto katika kujifunza masomo ya Sayansi.

"Ushiriki wa wanawake bado umekuwa kwa kiwango kidogo kutokana na changamoto za kimifumo ambazo ni katika mifumo ya utoaji wa fedha za kitafiti na kuna masuala ya mifumo ya utoaji elimu". Amesema Hildegalda.

Kwa upande wa fedha za kitafiti amesema kutokana na mila na destuli za kiafrika kuwa kuwepo na vigezo ambavyo vitamuwezesha mwanamke kupata mkopo na sio kuangajia jinsia ndio apate fedha hizo.

"Katika Utoaji wa Fedha  kuwepo na vigezo vitakavyoangalia je! hizi fedha za utafiti zinavyotoka zinawezaje zikafaidisha wanawake na wanaume kwa pamoja kwa sababu wakati mwingine mazoea ya mila na destuli za kiafrika,hata nchi za magharibi wamepita huko lakini wameweza kupita na kugundua yale mapungufu mbalimbali ambayo yamechukuliwa kuwa ni maisha ya kawaida basi wakaweza kugundua kuwa inasababisha mwanamke kuenguliwa katika kupata fedha za kitafiti, kwa kigezo hiki inahusika na jinsia na wala sio utaalamu".

Kwa upande wa Sera za nchi Hildegalda amesema kuwa miongozo ya kisera katika mabaraza yanayotoa fedha za kitafiti kuwe na vigezo na kuhakikisha kuwa mwanamke anapata nafasi ya kipekee ili waweze kufaidika na fedha za kitafiti.

Hata hivyo amesema kuwa  changamoto hizo zinaendelea hata katika taasisi za elimu ya juu na hata katika kusomea taaluma ya kitafiti changamoto zinaendelea kutokana na unyanyasaji wa kijinsia.

Katika mashauriano kwenye mkutano huo wameafikiana kuwa mwanamke anayefanya tafiti katika nchi 15 za kusini mwa jangwa la Sahara akikumbwa na unyanyasaji wa kijinsia ni lazima kutoa taarifa ndani ya siku 10 ili hatua cha kitafiti na kisheria ziweze kuchukuliwa.

"Kwa nchi ya Marekani wenzetu wamefanikiwa kwa mwanamke ambaye atafanyiwa ukatili wa kijinsia wakati akifanya utafiti wa kisayansi, kiteknolojia na ubunifu kutoa taarifa kwenye vyombo husika ndani ya siku 10 ili sheria ziweze kuchukuliwa kwa haraka sana na zimeanza kuzaa matunda".

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH), Profesa Mohamed Sheikhe amesema kuwa ili kuwa na watafiti waliobobea taasisi ya watafiti lazima iimarishwe iwekewe mipangilio bora na ziweze kuendelezwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad