BONGO ZOZO ALIPIA TIKETI 100 KWA WANAWAKE KUIONA TAIFA STARS - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 14 November 2019

BONGO ZOZO ALIPIA TIKETI 100 KWA WANAWAKE KUIONA TAIFA STARS

Raia wa Uingereza na mshabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kufuzu mataifa Afrika Afcon 2021 dhidi ya Equatorial Guinea kesho saa 1 kamili jioni.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Raia wa Uingereza na mshabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo amenunua tiketi 100 kwa ajili ya kuwapatia wanawake kwenda kuishangilia timu hiyo.

Bongo Zozo amesema kuwa wanawake wengi wanapokwenda uwanjani basi wachezaji wanafanya vizuri sana.

Akizungumza na waandishi wa habari   Bongo Zozo amesema ametoka nchini Uingereza amekuja Tanzania kwa ajili ya kuishangilia Taifa Stars na angependa kuona wanawake wengi wanajitokeza katika mechi hiyo.

Bongo Zozo amesema, ananunua tiketi 100 ili zigawiwe kwa wanawake na binafsi ataingia mtaani leo jioni na kuzigawa kwa wanawaje wote atakaokutana nao.

Amesema, yeye anapenda sana wanawake na anapenda kuona wanajaa uwanjani siku ya kesho.

"natoa hii hela, Katibu nanunua tiketi 100 kwa wanawake na ningependa nipate japo tiketi 50 ili nizigawe mweyewe, na kila mwanamke atakayeniona anidai tikeki yake,"amesema Bongo Zozo.

"nyie wenyewe mnajua, wanaume tukiwa wenyewe hapa tunakua kawaida ila wanawake wakiwepo utaona hadi tunagombana, na pia tumeshuhudia Iran alivyocheza na Cambodia wanawake waliruhusiwa kwa mara ya kwanza waliweza kushinda goli nyingi,"

Amesema, anaamini kesho Taifa Stars itashinda kwa goli nyingi na ameshajua mchezaji mmoja atakayefunga goli ambaye ni Farid Mussa na anaenda kambini muda huu kuongea nae na atamafundisha style ya kushangilia.

Bongo Zozo amekuwa ni moja ya mashabiki wazuri wa timu ya Taifa akishiriki kuwepo kwenye mechi nyingi sana pia amewataka wachezaji kushinda mchezo huo na iwapo hawatashinda basi wamrudishie nauli yake.

Kesho Taifa Stars wanashuka dimbani kucheza mchezo wa kwanza na Equatorial Guinea ikiwa ni mchezo wa kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon na mchezo wao wa pili utakuwa ni nchini Tunisia Novemba 20.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad