KAMPUNI YA MONMAR AND SONS YAKATALIWA KUPEWA MKATABA WA UJENZI WA MTANDAO WA MAJI SIKONGE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 5 November 2019

KAMPUNI YA MONMAR AND SONS YAKATALIWA KUPEWA MKATABA WA UJENZI WA MTANDAO WA MAJI SIKONGE

NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI imepiga marufuku Kampuni ya Monmar and Sons ya Mkoani Tabora kupewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa usambazaji wa miundombinu ya maji katika Vijiji vinne vya Kata ya Kitunda wilayani Sikonge kutokana na kutoridhishwa na ubora wa kazi zake katika baadhi ya maeneo nchini.

Mradi huo ambao ulikuwa ni kujenga chujio la maji, ujenzi wa tenki la maji na ujenzi wa mtandao wa usambazaji wa maji , kwa gharama za awali ulikuwa ugharimu shilingi milioni 900 lakini baada ya Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kufanya hesabu unatakiwa kutumia milioni 700.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Sikonge wakati wa ziara yake ya siku moja ya kusikilizia matatizo ya maji ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

Alisema katika maeneo mengi ambayo Kampuni hiyo ilipopewa miradi katika Mkoa wa Tabora na Katavi  ukakamilishaji wake umekuwa sio wa kuridhisha kwa kuwa imekuwa ikijengwa kwa kiwango cha chini na kuonekana na dosari muda mfupi baada ya kuzinduliwa.

Makame alisema mfano mzuri ni ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji cha Songambele wilayani Sikonge ambalo linavuja na kusababisha upotevu wa maji.

Aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kumchukulia hatua ikiwa ni pamoja na kumtaka kujenga upya tenki hilo na kumpa taarifa ndani ya wiki moja.

Aidha Profesa Makame alisema Wizara ya Maji itatoa shilingi milioni 250 za awali  kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mtandao wa kusambaza maji kutoka katika Bwawa la Igumila kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakazi wa Kata ya Kitunda.

Aliwataka kutumia mafundi jamii wakati wa utekelezaji wa mardi huo ili kupunguza gharama za awali ambazo walikisia kutumia milioni 900.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri alisema ni lazima ndani ya kipindi alichoagiza Waziri wa Maji kuhusu kufanyia marekebisho kasoro katika mradi wa Kijiji cha Songambele yanafanyika la sivyo atalazimika kumkamata la kumweka ndani.
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri akitoa taarifa ya maendeleo ya upatikanaji wa  maji kwa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara yake jana
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri (aliyenyosha mkono) akitoa maelezo  kwa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya maji katika Bwawa la Utyatya  wakati wa ziara ya Waziri huyo  jana
 Bwawa la Utyatya ambalo ni chanzo cha maji kwa wakazi wa Sikonge MjiniNo comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad