HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 27, 2019

Kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Arumeru yafanikiwa kwa asilimia 100

Na Woinde Shizza, Globu ya Jamii- Arusha



Kampeni ya ujenzi Wa vyumba vya madarasa mapya 107 ilioanzishwa na Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro umekamilika na kupita malengo kwani wilaya hiyo na kuweza kujenga vyumba vya madarasa 149.

Akizungumzia kampeni hiyo Mkuu huyo Wa wilaya amesema kuwa kampeni hiyo ilianza Mara baada ya kuingia tu wilayani humo ambapo alikuta wilaya hiyo ikikabiliwa na tatizo la uhaba Wa vyumba vya madarasa.

"Nikizungumzia sekta ya Elimu katika wilaya ya Arumeru kama mtakumbuka nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Tarehe 28/08/2019 Wilaya yenye Halmashauri mbili za Arusha Dc, na Meru Dc zenye jumla ya tarafa 6 na kata 53 Zenye Majimbo mawili ya Arumeru Mashariki na Magharibi,"

   "Moja kati ya kazi niliyoanza nayo ni kuanzisha kampeni ya ujenzi wa madarasa 107 mapya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi ujenzi ambao unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 2 na sasa tumeweza kujenga vyumba vya madarasa 149 badala ya 107" Amesema Muro

Amebainisha kubwa Katika Halmashauri ya Meru Vyumba 35 vya madarasa ya shule za msingi na Sekondari yamekamilika na Vyumba 42 vya madarasa ya sekondari na msingi vipo kwenye hatua za mwisho kukamilika.

Ameongeza kuwa ameweza kujenga Mejengo ya utawala mawili na yao katika hatua ya ukamilishaji, pamoja na Maabara mbili za science yakiwa hatua ya uezekaji , Pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo jipya na la kisasa la wadhibiti ubora wa Elimu .

Amesema kuwa hadi sasa imefikisha mwaka mmoja ambapo
katika Halmashauri ya Meru wameshajenga vyumba na majengo 82 

Na katika Halmashauri ya Arusha Madarasa yaliyokamilika 34 ambapo amesema yameanza kutumiwa kwa ajili ya sekondari na msingi na yaliyo katika hatua ya mwisho ni madarasa 73 kwa ajili ta shule za msingi na sekondari, katika Halmashauri ya Arusha jumla ya Madarasa 107 yanajengwa katika kampeni hiyo

Aidha ameabainisha kuwa Kampeni ya madarasa hayo mpaka sasa imewapa fursa ya kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 149 kutoka malengo ya kujenga vyumba 107, hivyo tumevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 100%

"Tumeweza kuongeza uandikishwaji,
Wilaya imefanikiwa kuongeza idadi ya wananfunzi wanaojiunga na elimu ya msingi, sasa katika wilaya ya Arumeru wananfunzi wote wanaopaswa kuanza elimu ya msingi wanaandikishwa kwa asilimia mia 

Amesema madarasa haya yamesaidia kwani hadi sasa Wilaya imeendelea kuongoza kwa kuwa wilaya ya kwanza kitaifa kwa ufaulu wa wanafunzi wa sekondari kidato cha sita (form six), na wako kwenye kumi bora kwa ufaulu kidato cha nne (form four)

"Naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mhe Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutusaidia fedha kwa ajili ya utoaji wa elimu Bure jambo ambalo limetusaidia kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa, pili Niwashukuru sana wakurugenzi wa Halmashauri za Meru Emanuel Mkongo na kwa upande Wa Arusha Dc Advera Nbabagoye na mtangulizi wake Mhe Dkt. Charles wilson Mahera , pi waheshimiwa madiwani kwa kuridhia utoaji wa vifaa na fedha kidogo " amesema muro

Aidha, Muro amewashukuru pia ubalozi wa Japani ambao umewasaidia zaidi ya milioni 100, pamoja na wadau wote wa maendeleo , viongozi wa dini na wananchi ambao wamesimama na sisi katika kipindi hiki cha kuweka msingi wa Maendeleo ya elimu katika wilaya ya Arumeru

 Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na walimu baada ya kutembelea majengo yaliyojengwa kwa ajili ya matumizi ya shule kupita malengo ya wilaya hiyo na kuweza kujenga vyumba vya madarasa 149.

Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikagua moja ya darasa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad