CBE WAZINDUA KATIBA YA UMOJA WA WAHITIMU WA CHUO HICHO (ALUMNI) - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 1 November 2019

CBE WAZINDUA KATIBA YA UMOJA WA WAHITIMU WA CHUO HICHO (ALUMNI)

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
CHUO cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) kimezindua rasmi umoja wa wahitimu waliosoma katika Chuo hicho katika matawi ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya na hiyo ni pamoja na kuzindua katiba ambayo itaongoza jumuiya hasa katika kutoa mchango wao katika masuala ya elimu na maendeleo kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye Afisa Biashara mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) na  mhitimu wa chuo cha CBE, Ally  Mayay  Tembele ameupongeza uongozi wa Chuo hicho na wahitimu wa chuo hicho kwa kuona umuhimu wa umoja huo utakaoongozwa kwa katiba maalumu.

Amesema kuwa licha ya kutambulika zaidi katika soka ila elimu ya biashara anayoifanyia kazi ameipata katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) hivyo umoja huo una manufaa na mafanikio kwao na kwa taasisi hiyo.

Mayay amesema Serikali ya awamu ya tano chini uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli na wasaidizi wake wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha taifa linajenga uchumi na viwanda ambao kupitia maarifa ya Elimu ya Biashara yanayotolewa na Chuo hicho yatafanikisha kwa kiasi kikubwa kuyafikia malengo hayo.

Amesema wahitimu lazima watumie fursa mpya zinazojitokeza hasa katika viwanda na hiyo ni kutokana na dira ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati kufikia mwaka 2025 na hiyo ni pamoja na kujishughulisha na masuala ya usindikaji wa mazao hasa ya kilimo ili kuweza kudhihirisha nguvu zao na maarifa yao katika kutenda kazi.

Kwa upande wake  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Emmanuel Mjema amesema kuwa na umoja wa wahitimu ni muhimu kwa kuwa hadhi ya Chuo hicho kipo juu kitaifa na kimataifa katika taaluma.

Aidha ameishukuru  Serikali kwa kuendelea kushiriki katika kuhakikisha kampasi zote za Chuo hicho zinapata mahitaji yote muhimu ili kuwezesha kupata elimu bora zaidi na amewashauri wahitimu hao kusaidiana hasa katika masuala ya kujiajiri na na kushirikiana na Chuo kwa kuwa mabalozi bora katika jamii.

Pia aliyekuwa Rais wa chuo hicho Jonathan  Nkwabi amesema kuwa wahitimu wa miaka iliyopita kutoka chuo hicho (Alumni) lazima washirikiane katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko na maendeleo katika chuo chao na hiyo ni pamoja na kuisaidia Serikali katika kufikia uchumi wa viwanda na hiyo ni kwa kuwa Chuo hicho ni hazina yakubwa ya masomo ya Elimu ya  Biashara.

Amesema kuwa umoja huo lazima ulete mabadiliko katika Chuo cha Biashara (CBE) na hiyo ni pamoja na kukishauri Chuo juu ya mwenendo wa ajira ili kuweza kurekebisha mitaala kulingana na mahitaji ya soko la ajira.

Nkwabi amesema kuwa umoja huo umesaidia katika kushiriki shughuli mbalimbali ya kijamii ikiwemo kutembelea wagonjwa, gereza la watoto upanga na kutembelea watoto yatima na hiyo ni pamoja na kuwa na wiki ya ubunifu pamoja na kutangaza shughuli mbalimbali wanazozifanya licha ya kupambana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wahitimu kutotambua faida ya kuwepo kwenye umoja huo.

Mmoja wa wahitimu kutoka Chuo hicho Renatha Rubaragamu aliyehitimu mwaka 1976 amesema kuwa Chuo hicho kimekuwa hazina kubwa katika masuala ya biashara na hata sasa chuo hicho kimeendelea kujiweka katika nafasi nzuri na kupitia umoja huo wanaamini watafika mbali zaidi.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni  Afisa Biashara mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) na  mhitimu wa chuo cha CBE, Ally  Mayay  Tembele akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa katiba itakayoongoza umoja wa wahitimu wa Chuo hicho, leo jijini Dar es Salaam. 
Mgeni rasmi ambaye pia ni  Afisa Biashara mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) na  mhitimu wa chuo cha CBE, Ally  Mayay  Tembele akiwa na viongozi mbalimbali wa Chuo hicho wakionesha katiba ambayo itaongoza umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni,) leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi  Afisa Biashara mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) na  mhitimu wa chuo cha CBE, Ally  Mayay  Tembele akizungumza katika hafla yaa kuzindua katiba ya umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) na kueleza kuwa maarifa yanayotolewa na Chuo hicho  yana tija kubwa katika kufikia uchumi wa kati kwaka 2025, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Emmanuel Mjema akizungumza katika hafla hiyo ya kuzindua katiba ya umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) ambapo amesema kuwa wahitimu lazima wawe mabalozi bora kwa Chuo hicho pamoja na kusaidiana katika masuala ya kujiajiri wenyewe, leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE) anayeshughulikia masuala ya  Fedha, utawala bora na Mipango Dkt. Emmanuel Munishi akizungumza katika hafla ya kuzindua umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) ambapo ameeleza kuwa wanaamini umoja huo utaleta mapinduzi hasa katika sekta ya elimu na maendeleo kwa ujumla,  leo jijini Dar es Salaam.
 Mhitimu wa Chuo cha Biashara (CBE) mwaka 1976, Lenatha Rubaragamu akizungumza katika hafla hiyo ya kuzindua umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) na kueleza kuwa maarifa aliyoyapata kutoka Chuo hicho yamekuwa hazina kubwa katika utendaji kazi wake, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Leonidas Tibanga akisherehesha hafla hiyo ya uzinduzi wa katiba ya umoja wa wahitimu wa chuo hicho, leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wahitimu (Alumni) waliohitimu kuanzia mwaka 2018 kurudi nyuma hadi mwaka 1965 wakichangia mada kwenye mkutano wa uzinduzi wa katiba ya umoja huo uliofanyika katika hoteli ya Peacock leo jijini Dar es Salaam


Baadhi ya wahitimu (Alumni) waliohitimu kuanzia mwaka 2018 kurudi nyuma hadi mwaka 1965 wakiwa katika hafla hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
 Kikundi cha sanaa cha One Group wakitumbuiza katika hafla ya kuzinduakatiba ya umoja wa wahitimu wa Chuo cha biashara (CBE), leo jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad