Bibi aliyemuua mjukuu wake kwa kipigo ahakumiwa kunyongwa hadi kufa - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 8 November 2019

Bibi aliyemuua mjukuu wake kwa kipigo ahakumiwa kunyongwa hadi kufa

Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mwanamke Esther Lyimo (47) baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mjukuu wake Naomi John (7) kwa kipigo

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 8, 2019 na Naibu  Msajili wa Mahakama Kuu Pamela Mazengo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji baada ya kuridhika na ushàhidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashitaka na utetezi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mazengo amesema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa kifo cha naomi kimetokana na kipigo na majeraha ya bibi yake hivyo ametiwa hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Naomi John.

Hakimu Mazengo amesemà  "adhabu katika kosa la mauaji ni moja tu ni kunyongwa hadi kufa," hivyo mahakama inakuhukumu kunyongwa hadi kufa" amesema.

Awali kabla ya kuhukumiwa mshitakiwa katika utetezi wake, aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu hilo ni kosa lake la kwanza pia ana familia inayomtegemea na amekaa gerezani miaka 3.

Hata hivyo upande wa mashitaka uliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo ya kuwafanyia watoto ukatili.

Mapema jana mchana, wazee wa baraza katika kesi hiyo, waliiomba mahakama kumtia hatiani mshtakiwa kwa mauaji ya kukusudia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wazee hao wa walitoa maoni yao kwamba kutokana na ushahidi wa Andrew John (9) ambaye alishuhudia tueekio la kupigwa kwa marehemu Naomi John inaonesha wazi mshtakiwa alikusudia kufanya mauaji.

Walidai watoto walikuja Dar es Salaam kwa ajili ya kusoma lakini malengo hayo hayakutekelezeka kwa sababu watoto, Naomi na Andrew hawakupelekwa shule matokeo yake walikutana na huo ukatili wa kuteswa na kunyanyaswa na mshtakiwa ambae alikuwa mama wa ubatizo wa mtoto Naomi (marehemu)

Wamedai, Kulingana na ripoti ya daktari iliyoonyesha marehemu alikutwa na majeraha mwilini huku mshtakiwa mwenyewe alikiri kiwa alimchapa marehemu kwa fimbo ya mpera, hiyo inaonesha wazi kuwa aliua kwa kukusudia.

Moja ya ushahidi wa upande wa mashtaka ulidai kuwa, mshtakiwa alimpiga marehemu, kumng'ata mwilini na kisha kumwagia maji ya moto ya chai ambapo inadaiwa ilikuwa tabia yake kuwafanyia ukatili watoto hao Andrew na marehemu Naomi.

Katika utetezi wake mshtakiwa huyo ameiomba mahakama imuonee huruma na kumuachia huru  huku akidai alikuwa akimchapa marehemu kwa kumkanya na kwamba vidonda na makovu aliyokutwa nayo mwilini alitoka nayo kijijini kwao mkoani Kilimanjaro sababu alikuwa anachunga mbuzi.

Akielezea jinsi namna marehemu Naomi na Andrew John wanavyomuhusu alidai ni
ni watoto dada yake na aliwachukua kuishi nao baada ya kuombwa awasomeshe  kwa kuwa dada hakuwa na uwezo ambapo aliishi nao nyumbani kwake Tuangoma Kigamboni kwa takribani miezi kumi.

ai aliweza kukaa na watoto hao kwa miezi 10 nyumbani kwake Twangoma mbako pia kuna mapori kama kijijini kwao  Moshi.

"Watoto hao ni watundu sana, huwa wanakimbizana na kucheza vichakani ambako huku nako kuna mapori kama kilimanjaro hivyo ndio maana mwili wake ulikuwa na vidonda na makovu, sijamuua Naomi, nilikuwa nawapenda , naomba mahakama iniachie huru.

"Machi 25, mwaka 2016 wakati natoka kufanya usafi Saloon kwangu,  nilielezwa na Andrew kuwa Naomi ameamka, amejikojolea yupo barazani. Nilipoingia ndani nlimwambia Naomi akapige mswaki, lakini aliendelea kukaa barazani , Andrew akaniambia tena hapigi mswaki anachezea maji, nikaongea kwa sauti kwamba nikitoka ndani nitàmchapa, nilipotoka Naomi akakimbia nikamwambia Andrew amkamate.

" Alipoletwa nilichuma fimbo katika mti wa mparachichi na kumchapa kwa nia ya kumkanya kama mzazi, wakati namchapa Naomi akasema amechoka, mi nilizani ni utani kwasababu ya kukimbia na ujeuri wake, nilimnyànyua na kumweka barazani, nikaenda kutafuta dawa, nilivyorudi nilikuta amelegea sana, nikachukua gari ya jirani na kumpeleka hospitali Temeke amapo daktari alitufahamisha kuwa Naomi alifariki duni

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad