HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 7, 2019

WANAFUNZI WAKEMEWA KUFANYA VISASI KWA WALIMU PAMOJA NA KUCHOMA MOTO SHULE-ALHAJ LASENGA

 Na Mwamvua Mwinyi
WANAFUNZI hususan wa shule za sekondari, wamekemewa kujiepusha kuweka visasi na walimu wao kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha madhara ikiwemo kuchoma moto shule husika na kurudisha nyuma maendeleo ya shule.

Pamoja na hilo ,wazazi na walezi wametakiwa ,kushirikiana na wawekezaji wa masuala ya elimu na kuacha kuwakwamisha katika juhudi hizo.

Akizungumza katika mahafali ya tano ya shule ya kiislamu ya sekondari ya Vuchama,iliyopo Ugweno Kilimanjaro, mlezi wa walimu BAKWATA Mkoa wa Kilimanjaro, Alhaj Sheikh Yusufu Lasenga 
 Alisema ,baadhi ya shule nchini zimekuwa zikichomwa moto na wanafunzi ambapo kwa upande mwingine inatokana na visasi visivyokuwa na tija kwa maendeleo ya kielimu.

"Jiepusheni migongano na walimu wenu, usiweke tofauti kisa mmechapwa viboko ama mmeonywa na walimu kwakuwa nao ni sehemu ya wazazi wenu"alisisitiza Lasenga.

Lasenga aliwasihi, wanafunzi kuwa na nidhamu na maadili yaliyo mema ndani ya jamii ili kuinua taaluma zao.

Nae mkurugenzi  wa wakurugenzi wa shule zinazomilikiwa na Njuweni Institute, Yusuph Mfinanga hakusita kukemea baadhi ya wazazi na walezi wanaobagua kutoa elimu kwa watoto wakiume na wakike.
Mfinanga, aliomba ushirikiano na jamii katika jitihada zake za kuunga mkono juhudi za serikali kuinua sekta ya uwekezaji kwenye masuala ya elimu.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Vuchama, Jumanne Mkoga alisema shule hiyo inafanya vizuri kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo ambapo mwaka 2016 ilikuwa ya tatu kimkoa kati ya shule 33 na kitaifa 58 kati ya shule 1,439.

"Mwaka 2017 tulikuwa wa pili kimkoa kati ya shule 55 na kitaifa 32 kati ya shule 1,738 na mwaka 2018 tulikuwa wa kwanza kimkoa huku kitaifa tukiwa wa 22 kati ya shule 1,371.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad