NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI itapitia mkataba wa ubinafsishaji wa Kiwanda cha Nyuzi cha
Tabora (New Tabora Textile Tanzania Limited) baada ya kutoridhishwa
utendaji wa uzalishaji ili kuchukua hatua mapema ambazo zitasaidia
kufanyakazi kwa kiwango chake endapo itabainikiwa wawekwenda kinyume
kwa masharti yaliyomo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Viwanda na Bisahara Innocent
Bashungwa wakati wa ukaguzi wa viwanda mbalimbali mkoani Tabora na
kukuta kiwanda cha Nyuzi Tabora kikiwa katika uzalishaji mdogo wakati
pamba ya wananchi imejaa mitaani.
Alisema kiwanda hicho kingekuwa kinafanyakazi kulingana na uwezo wake
kingesaidia sana kupunguza tatizo la ununuzi wa pamba ya wakulima
kususua na kingeongeza uzalishaji wa zao hilo na kukuza uchumi wa Mkoa
na Taifa.
Bashungwa alisema kwa kuwa Mmiliki wa Kiwanda hicho ameonekana kuwa na
uwezo mdogo na hivyo awe tayari na maamuzi ambayo yatafikiwa baada ya
kuangalia mkataba na vigezo alivyopewa wakati ubinafishaji na
ikibainika amekiuka Serikali itachukua hatua ili kuongeza tija na
utendaji kazi wake.
Alisema wakati wa Mwekezaji huyo na wengine kuendelea kukalia viwanda
ambavyo vilitarajiwa kuzalisha kwa ajili ya kukuza uchumi na kutengeza
ajira umekwisha na Serikali itachukua hatua.
“Tutangalia Sheria inasemaje na mkataba mlioingia …ili kuangalia njia
bora ya kukifanya kiwanda hiki kifanye kazi kwa ajili ya mustakabali
mzuri wa wakazi wa Tabora na nchi kwa ujumla” alisema.
Aidha Waziri huyo alivitaja Viwanda vingine ambavyo uzalishaji na
utendaji wake sio mzuri ni pamoja na Mwatex na Mutex ambavyo navyo
mikataba ya ubinifsishaji wake itachunguzwa kwa ajili ya kuchukua
hatua kuvinusuru.
Awali Mbunge wa Tabora Mjini Emmenuel Mwakasaka alisema toka mwaka
jana alipotembelea Kiwanda hicho hakuna maendeleo yoyote ambayo
yamefanyika na kukifanya kutokuwa na tija kwa vijana na wakazi wa
Tabora.
Alisema toka mwaka jana hakuna ajira hata moja iliyoongezeka zaidi ya
mfanyakazi mmoja.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (aliyeshika uzi) akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Pascal Jotham (mwenye shati nyeusi) leo alipokuwa Mkoani Tabora kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (katikati ) akiwa ameshika mmoja ya kitambaa kilichozalishwa na Kiwanda cha Nyuzi Tabora wakati wa ziara yake Mkoani Tabora jana ya kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa(kushoto) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(kulia) wakati wa ziara yake Mkoani Tabora jana ya kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda cha Nyuzi Tabora na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (mwenye shati nyeupe) akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Pascal Jotham (mwenye shati nyeusi) leo alipokuwa Mkoani Tabora kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake. PICHA NA TIGANYA VINCENT
No comments:
Post a Comment