DC ILEJE AZINDUA CHANJO YA POLIO NA SURUA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 17 October 2019

DC ILEJE AZINDUA CHANJO YA POLIO NA SURUA

 Na Daniel Mwambene, Ileje
Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe leo amezindua zoezi la chanjo ya surua,lubela na polio akiwataka wananchi kutoficha watoto ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la soko katika kijiji cha Itumba huku zoezi hilo la kitaifa likifanyika tangu saa mbili asubuhi kwenye maeneo mengine ya wilaya hiyo na nchi nzima.
Awali,akisoma taarifa kwa Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,Dkt.Enock Mwambalaswa alisema kuwa zaidi ya watoto 28 wataweza kufikiwa na zoezi hilo likitarajiwa kufanyika kwa siku tano.

Dkt.Mwambalaswa alisema kuwa wakati wa zoezi hilo watoto 17,783 watapata chanjo ya surua  huku watoto 10795 wakipata chanjo ya polio wote wakiwa na umri wa miezi tisa hadi 59.
Zoezi hilo lilitanguliwa na mafunzo ya siku moja kwa wahudumu wa afya 83 yaliyofanyika Itumba kwa Tarafa ya Bulambya na Isoko kwa Tarafa ya Bundali.

Wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Herman Njeje aliwataka wahudumu hao kutoa huduma itakayowezesha Wizara kufikia malengo yake.
 Mkuu wa Wialaya ya Ileje Ndg. Joseph Mkude akizindua zoezi la chanjo ya polio,surua na lubela,hapa ni katika eneo la soko Itumba,mbele yake ni mzazi akiwa na mtoto wake aliyekuwa wa kwanza kuchanjwa siku hiyo.
 Dc wa Ileje Ndg.Joseph Mkude akiwa amembeba mtoto Ivan Lukumay aliyekuwa wa kwanza kuchanjwa siku ya uzinduzi wa chanjo kiwilaya mjini Itumba.
 Wazazi na walezi wa Itumba-Ileje wakiwa kwenye foleni wakisubiri watoto wao wapewe chanjo ya polio,lubela na surua.
 Dc mkude wa Ileje akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa chanjo kiwilaya katika mji wa Itumba.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ileje wakifurahia jambo siku ya uzinduzi wa chanjo ya polio,surua na lubela.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad