HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 14, 2019

DAWASA WAMPONGEZA ENG. ARON JOSEPH KWA UTEUZI WA KAIMU MKURUGENZI MUWSA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishani na Usambazaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam  (DAWASA) Mhandisi Aron Joseph ambaye ameteuliwa na Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) umempongeza Mhandisi Aron Joseph kwa kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).

Uteuzi huo umefanyika jana na Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa kwa Kuwatangaza wakurugenzi wa Mamlaka za maji na Usafi wa mazingira za miji mbalimbali nchini

Mpaka anateuliwa nafasi hiyo, Aron amekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishani na Usambazaji wa Mamlaka ya Dawasa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja sambamba na Menejimenti nzima wamempongeza Mhandisi Aron kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hiyo na zaidi wanajivunia kuweza kumtoa kiongozi mwingine kwa ajili ya miji ya Tanzania.

Aidha, Aron anaenda kuchukua nafasi ya Joyce Msiru aliyemaliza muda wake.

Uteuzi mwingine uliofanywa na Waziri Mbarawa ni pamoja Mhandisi Ndele Mengo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya UWSSA) akichukua nafasi ya Mhandisi Simon Shauri.

Uteuzi mwingine ni Mhandisi Justine Rujumba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) akichukua nafasi ya Mhandisi Ruth Kayo na Mhandisi Leonard Misenyele ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWSA) akichukua nafasi ha Mhandisi Anthony Sanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad